Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rodriguez ala umeme, ‘pufya’ yamponza

RODRIGUEZ Pict

Muktasari:

  • Kesi hii inatoa funzo muhimu kwa wanamichezo wote kuwa mpango wa kutumia dawa za kusisimua misuli unaweza kuharibu mafanikio, ukitumia dawa hizo, ushindi unaweza kupotea na hata kufungiwa kama ilivyokuwa kwa bondia huyo wa Mexico.

GUADALAJARA, MEXICO: BONDIA wa Mexico, Francisco Rodriguez Jr, amefungiwa kushiriki mchezo wa ngumi kwa miaka miwili kufuatia kukutwa ametumia dawa zilizopigwa marufuku (pufya) baada ya pambano lake dhidi ya Galal Yafai lililofanyika Juni 2025 nchini Uingereza.

Katika pambano hilo, Rodriguez alionyesha uwezo kubwa kwa kumwangusha Yafai, mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki, kabla ya kushinda kwa uamuzi wa majaji baada ya raundi 12 na kutwaa taji la WBC uzito wa flyweight.

Hata hivyo, ushindi huo haukudumu. Baada ya vipimo kufanyika, ilibainika kuwa Rodriguez alitumia dawa zilizopigwa marufuku. Kutokana na matokeo hayo, WBC ilibatilisha ushindi wake na kutangaza pambano hilo kuwa halina matokeo rasmi huku Yafai akirejeshewa hadhi yake ya bingwa.

RODRI 01

Uchunguzi wa kina ulionyesha kuwa mwilini mwa Rodriguez kulikuwemo octodrine, heptaminol na oxilofrine dawa ambazo haziruhusiwi kutumika wakati wa mashindano. Matokeo haya yalisababisha hatua za haraka kutoka Shirika la Kupambana na Dawa Haramu la England (UKAD).

Rodriguez hakutoa majibu yoyote kwa mamlaka husika licha ya kuwasiliana naye mara kadhaa. Aidha, alishindwa pia mtihani mwingine wa dawa mwezi Desemba 2025, jambo lililosababisha kupewa adhabu ya kufungiwa kwa miaka miwili.

Kwa mujibu wa uamuzi wa UKAD, Rodriguez amefungiwa kwa miaka miwili kuanzia Julai 30, 2025 na marufuku hiyo itamalizika Julai 29, 2027. Hii inamaanisha kuwa hatoweza kushiriki mashindano yoyote hadi wakati huo.

Bondia huyo ana rekodi ya ushindi wa mapambano 41, kupoteza 6 na sare 1.        Pia Amewahi kushindania mataji ya dunia katika uzito wa super flyweight na light flyweight, lakini hakukushinda.

RODRI 02

Hata hivyo, alishinda mataji ya dunia katika uzito wa minimumweight mwaka 2014, akipata mataji ya IBF na WBO.

Kwa upande mwingine, Galal Yafai bado hajapoteza katika rekodi yake ya mapambano ya kulipwa, baada ya matokeo yake dhidi ya Rodriguez kubatilishwa. Yafai sasa anatarajiwa kupambana na bingwa wa dunia wa uzito wa flyweight, Ricardo Sandoval, katika pambano lijalo.

Kesi hii inatoa funzo muhimu kwa wanamichezo wote kuwa mpango wa kutumia dawa za kusisimua misuli unaweza kuharibu mafanikio, ukitumia dawa hizo, ushindi unaweza kupotea na hata kufungiwa kama ilivyokuwa kwa bondia huyo wa Mexico.