Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rocky: Bingwa wa dunia aliyegeuka ombaomba - Sehemu ya pili

Rocky Pict
Rocky Pict

Muktasari:

  • Lockridge anasema pia hakuwa anapata pesa nyingi kama malipo ya mapambano yake jambo ambalo Kathy Duva alithibitisha akisema, bondia huyo hakupata pesa ambazo zingemfanya kuishi milele bila ya shida yoyote na pambano ambalo lilimpa pesa nyingi zaidi lilikuwa ni lile dhidi ya Chavez, ambalo alipata Dola 200,000.

KATIKA sehemu ya kwanza tuliona kwa ufupi juu ya maisha ya bondia Mmarekani Rick Lockridge maarufu kama “Rocky” ambaye aliwahi kuwa bingwa wa super-featherweight akiutetea mara mbili kati ya mwaka 1984 hadi 1985 kabla ya kugeuka ombaomba.

Hadi anaachana na masumbwi alikuwa amepigana mapambano 53 akishinda 44 na kupoteza tisa.

Rocky anasimulia jinsi alivyokuwa akinywa kila aina ya pombe iliyokuwa mbele yake na kutumia dawa za kulevya kila baada ya pambano.

Baadaye alipata ajali kutokana na kuendesha gari akiwa amelewa na akapata kiharusi hivyo sehemu ya mwili wake ikapooza. Kipato kikakata, akajikuta ameingia mtaani kuwa ombaomba.

Endelea...


Lockridge anasema pia hakuwa anapata pesa nyingi kama malipo ya mapambano yake jambo ambalo Kathy Duva alithibitisha akisema, bondia huyo hakupata pesa ambazo zingemfanya kuishi milele bila ya shida yoyote na pambano ambalo lilimpa pesa nyingi zaidi lilikuwa ni lile dhidi ya Chavez, ambalo alipata Dola 200,000.

“Alikuwa na familia, watoto na alinunua nyumba,” anasema Kathy Duva. “Pesa hupotea. Watu wanaotumia dawa za kulevya mara nyingi huishia katika shida kubwa. Ni aibu, lakini ni chaguo wanalochagua.”

RO01
RO01

Baada ya kufeli katika mapambano mawili aliyojaribu kupigana baada ya kurejea kutoka kustaafu, mwaka 1992, Rocky, hatimaye alistaafu rasmi masumbwi.

Nia yake ya kutaka kurejea tena ulingoni ilishindikana kwani miezi kadhaa baadaye baada ya kutangaza kuachana na mchezo huo alipata ajali mbaya ya gari iliyosababisha apate jeraha la kichwa.

Ajali hiyo ambayo ilisababishwa na kuendesha akiwa amelewa ilimtingisha sana kiafya na pia akapatwa na kiharusi na tangu hapo hakuweza tena sio tu kupigana bali hata kuwa mwalimu wa mabondia wengine.

Hakuwa anaingiza chochote tena na kila siku zilivyozidi kwenda maisha yalikuwa magumu kwani familia ya watoto wawili aliyokuwa nayo ilihitaji huduma na pia kulikuwa na bili mbalimbali za kulipa.

Baada ya mwaka mmoja na nusu Rocky, mkewe Carolyn na watoto wao wawili mapacha walirejea Tacoma, Washington ambako mambo yalikuwa magumu zaidi.

Muda mfupi tu baada ya kufika Tacoma, Rocky na Carolyn walitalikiana na Lockridge aliamini kwamba moja ya sababu za suala hilo kutokea ilikuwa ni yeye mwenyewe kwani wakati huo alikuwa ameanza kuzidisha utumiaji wa dawa za kulevya na hakuwa na pesa kwani hakuweza kupanda ulingoni kutokana na afya yake.

Miezi kadhaa baada ya kutalikiana mwaka 1993, Lockridge akiwa na umri wa miaka 34, alihamia Camden peke yake ikiwa ni baada ya talaka na kutengana na familia yake.

“Sikuweza kujihusisha na masuala ya masumbwi, sio tu kutokuwa mpigaji sikuweza hata kushiriki kama promota au mkufunzi, mke wangu Carolyn na mimi wote tulipata pigo, aligundua kwamba nisingeweza  kuvumilia na kupambana na hali hiyo, mimi na yeye tuliona kwamba tusingeweza tena kuwa pamoja na kushirikiana kama ilivyokuwa hapo awali,” alisema Lockridge juu ya mkasa wake wa kuachana na mkewe na kurejea Camden.

RO02
RO02

Baada ya kuwasili Camden, Lockridge alianza kufanya kazi katika kampuni ya William Jones & Son, Inc. ambayo ni kampuni inayotengeneza  mapipa na madumu kwenye Mtaa wa Liberty, ambako alikuwa akisafisha na kupaka rangi mapipa na alilipwa Doa 8 kwa saa akianza rasmi Januari 1994.

Akiwa anafanya kazi hiyo pia aliingia katika tabia ya kuwa mwizi ambapo alikamatwa mara ya kwanza kwa kosa la wizi wa majumbani na akahukumia kifungo cha nje lakini haikuchukua muda mrefu akaiba tena na kukamatwa, baada ya hapo alihukumiwa kwenda jela miezi 27 kabla ya kuachiliwa huru mwaka 1999.

Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani hakwenda tena kazini, na aligundua kwamba hakuwa na sehemu ya kuishi mwishowe akaishia mitaani.

“Sijui hasa kilichotokea kwa wakati huo katika maisha yangu,” alisema Lockridge ambaye anafunguka kwamba baada ya hapo alichokifanya ni kurudi tu katika matumizi ya dawa za kulevya.

“Nilijua watu wengi niliokuwa nasheherekea nao hapa Camden mara baada ya kupata ushindi wa pambano fulani.”

Lockridge anasema kwamba ikiwa utaamua kuishi mitaani, basi Camden ndiyo mahali pekee panapofaa kwa sababu kuna maeneo mengi ambayo yatakupa mlo bure, na hifadhi nyingi ambazo zitakuwezesha kulala kwa usiku mmoja.

Lockridge alikuwa akiishi kwa kiasi cha dola 140 kwa mwezi alichokuwa anapewa na serikali pia alikuwa anapata pesa kwa kuombaomba.

Sehemu aliyotumia kulala ilikuwa ni hifadhi maalumu zilizotengwa na serikali ambazo zilikuwa zinaruhusu watu wasio na makazi kulala kwa usiku mmoja.

Mwenyewe alifunguka kwamba hali ya kulala katika sehemu hizo sio nzuri kutokana na wingi wa watu na kuna muda alikuwa aking’atwa na wadudu.


OMBA01
OMBA01

HAKUPEWA MSAADA?

Taasisi ya mabondia wastaafu ilisema itamsaidia lakini kwa sharti la kuachana na ulevi na kukubali kuondoka katika malazi ya serikali anakolala.

“Rocky angeweza kuwa na haki ya kupata pesa kutoka kwa taasisi ambayo angepokea kama hundi ya kila mwezi, makazi na huduma ya matibabu lakini moja ya masharti ni kwamba aache ulevi,” alisema Jacquie Richardson, mkurugenzi mtendaji wa RBF. “Mabondia mara nyingi hawapendi kukubali msaada. Huona ni aibu kubwa. Wanajutia kuona hawakujiandaa na maisha baada ya kupigana, hushindwa kabisa kujisamehe, mwisho wanaamua kujificha huko waliko.”

Ilipofika mwaka 2010, kwa msaada wa chama cha mabondia wastaafu, Rocky alikutanishwa na familia yake kupitia kipindi cha televisheni cha Intervention.

Mahojiano yake yalisambaa sana na watu wengi wakaguswa na hali yake, mwishowe Lockridge alikubali kuacha ulevi na akaanza rasmi matibabu ya kuacha uraibu.

“Nitarejea katika utimamu wangu na kuacha dawa za kulevya,” alisema Lockridge katika mahojino yake mwaka 2010 mara baada ya kukutanishwa na familia yake.

“Nina familia ambayo nataka kuwa nayo hadi wakati wangu utakapomalizika hapa duniani. Nina jukumu hilo kwa sasa, watoto wangu na familia kwa ujumla inanitaji.”

Video yake inayomuonyesha akimwaga kilio katika mahojiano hayo ya televisheni alipokutanishwa na familia yake imekuwa maarufu sana hadi sasa. Kilio hicho kimekuwa kikitumiwa katika mitandao ya kijamii (pengine bila ya kujua) kama sehemu ya utani pale inapotokea labda mtu ameteleza na kuanguka, kisha inawekwa video ya Rocky alivyomwaga kilio hicho, ambacho wengine hudhani ni igizo.


OMBA02
OMBA02

KUPOTEZA MAISHA

Baada ya kukaa muda mrefu katika nyumba ya watu wanaopambana kuachana na uraibu wa dawa za kulevya, Lockridge alifariki dunia Februari 7, 2019, akiwa na umri wa miaka 60, baada ya kupelekwa katika kituo cha uangalizi kutokana na hali yake kuwa mbaya. Alizikwa huko Pennsauken, New Jersey.