Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Riyad Mahrez apuuza wakosoaji Algeria

Muktasari:

  • Mahrez, anayekipiga klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia baada ya kuondoka Manchester City, alifunga mabao mawili mjini Rabat, Morocco kabla ya Ibrahim Maza kufunga bao lake la kwanza la kimataifa.

NAHODHA wa Algeria, Riyad Mahrez, amesema mabao mawili aliyofunga katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Sudan juzi usiku kwenye mechi ya Kundi E ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) hayakuwa jibu kwa wakosoaji wake.

Mahrez, anayekipiga klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia baada ya kuondoka Manchester City, alifunga mabao mawili mjini Rabat, Morocco kabla ya Ibrahim Maza kufunga bao lake la kwanza la kimataifa.

Nyota hiyo mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Algeria katika AFCON akiwa na mabao manane.

Hata hivyo, amekuwa akikabiliwa na ukosoaji baada ya Desert Warriors waliokuwa mabingwa wa michuano hiyo wa 2019, michuano ilipofanyika Misri kwa kuifunga Senegal katika fainali kutolewa katika hatua ya makundi kwenye mashindano mawili yaliyopita huko Ivory Coast.

“Hii haikuwa kuhusu kujibu ukosoaji,” Mahrez aliwaambia waandishi wa habari. Nimezoea hilo.

“Jibu langu ni kuzingatia mchezo wangu uwanjani. Tuliingia tukiwa na mpango kazi wa kucheza bila kuwaza sana, kushinda mechi hii na mechi zingine za kundi letu ili kurahisisha njia,” alisema Mahrez.

Algeria iliyokosa kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mara mbili zilizopita, safari hii tayari imekata tiketi kwa Kombe la Dunia la 2026 litakalofanyika Marekani, Mexico na Canada.

Mahrez yupo Morocco akiwa ametoka kushinda taji la AFC Champions League Elite (jina jipya la mashindano) akiwa na Al Ahli mwaka huu, baada ya klabu hiyo ya Jeddah kuifunga Kawasaki Frontale ya Japan 2-0 na kutwaa taji lao la kwanza la bara hilo.

“Ni vizuri kufunga mabao kunaleta kujiamini,” alisema staa huyo.

“Lakini timu inapaswa kuendelea kuinua kiwango chetu ili tuwe na uthabiti zaidi,” alisema Mahrez na kuongeza; “Sasa tunalenga Burkina Faso. Tunahitaji kuboresha mchezo wetu na kuwa imara zaidi kuanzia mechi ijayo.”

Algeria inaongoza Kundi E kwa pointi tatu na itacheza dhidi ya Burkina Faso keshokutwa Jumapili.

Awali, juzi alasiri Burkina Faso ilifunga mabao mawili mwishoni mwa muda wa nyongeza kipindi cha pili na kuifunga Equatorial Guinea 2-1, licha ya Guinea hiyo kubaki na wachezaji 10 uwanjani.