Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ripoti ya ajali ya Jota ni hii

JOTA Pict

Muktasari:

  • Ripoti ya awali iliyotolewa Jumanne ilieleza huenda gari hilo lilikuwa kwenye mwendokasi wakati lilipopata ajali ambayo ilisababisha kuungua moto na kusababisha vifo vya wachezaji hao wawili wa soka.

ZAMORA, HISPANIA: DEREVA wa lori ambaye inadai aliona gari aina ya Lamborghini la Diogo Jota na Andre Silva likiwaka moto ameihakikishia familia ya ndugu hao kuwa gari hilo halikuwa likiendeshwa kwa mwendo kasi wakati ajali ilipotokea.

Ripoti ya awali iliyotolewa Jumanne ilieleza huenda gari hilo lilikuwa kwenye mwendokasi wakati lilipopata ajali ambayo ilisababisha kuungua moto na kusababisha vifo vya wachezaji hao wawili wa soka.

Wachunguzi wa ajali wamekuwa wakichambua alama zilizoachwa na matairi ya gari hilo, huku kukiwa na tetesi moja ya tairi lililipuka. Polisi walisema katika taarifa yao wanajaribu kubaini kama ni mwendokasi uliosababisha ajali hiyo.

Video ya tukio hilo imetolewa saa chache baada ya kufichuliwa dereva mwanamke karibu apoteze maisha kwenye barabara hiyo hiyo hatari siku hiyo hiyo kabla ya ajali ya Jota kutokea.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 alipata majeraha makubwa katika eneo la kilomita 65, kwenye barabara hiyo hiyo aliyopita Jota, Jumatano iliyopita saa 5:30 asubuhi (kwa saa za eneo Hispania).

 kwa mujibu wa taarifa ya tovuti AS ya huko Hispania Gari lake lilitoka barabarani na akapata ajali kabla ya baadaye kusaidiwa na watu wa uokozi na kupelekwa hospitalini.

Dereva wa lori, Jose Azevedo ambaye amesema alirekodi video ya eneo hilo akiwa ndani ya gari lake aliiambia familia ya wachezaji hao gari la Jota halikuwa linaendesha kwa mwendokasi wakati ajali ilipotokea.

Amesema: “Nilirekodi, nikasimama, nikajaribu kusaidia, lakini kwa bahati mbaya, sikuweza kufanya kitu. Nilikuwa na dhamira safi. Najua nilichopitia usiku ule kwa sababu sikujua ni nani aliyekuwa ndani ya gari. Pole kwa familia na niwaambie tu kuwa hawakuwa kwenye mwendo kasi. Niliweza kuona aina ya gari na rangi ya gari.”

“Huwa napita barabara hii kila siku, kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi. Najua barabara hii ni ya hatari sana,

Ni barabara ya giza, niliona kila kitu vizuri kuanzia aina na rangi ya gari. Baadaye, kwa bahati mbaya ajali ndio ikatokea.”

Jota, 28, alikuwa akisafiri na ndugu yake mdogo, Silva (26), karibu saa 6:35 usiku (kwa saa za eneo hilo) na inasemekana tairi ya Lamborghini Huracan alilokuwa anaendesha lilipasuka walipokuwa wakijaribu kuipita gari iliyokuwa mbele yao maeneo ya barabara ya A-52, Cernadilla, karibu na Zamora, Kaskazini Magharibi mwa Hispania, karibu na mpaka wa Ureno.

Gari hilo lenye rangi ya kijani kibichi  lilitoka barabarani na kupinduka kabla ya kulipuka kwa moto, ambao pia uliteketeza maeneo ya kichaka yaliyokaribu.

Vikosi vya dharura vilifika haraka eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kuwaokoa ndugu hao.

Walikuwa katika safari ya kuelekea Santander, kaskazini mwa Hispania, ambako wangepanda kivuko na kuelekea England ikiwa ni baada ya Jota kupewa ushauri wa kutosafiri kwa ndege kufuatia upasuaji wa mapafu aliokuwa amefanyiwa.

Baada ya kifo cha Jota, mwakilishi wa serikali kuu katika mkoa wa Zamora alieleza barabara ya A-52 ni ‘hatari sana’.

Mwaka 2023 kulikuwa na ajali 19 kwenye barabara hiyo ya A-52 na kulingana na gazeti The Mirror, wastani wa vifo 1.5 vilirekodiwa kwa kila tukio.

Barabara hiyo inajulikana pia kuwa na mashimo mengi ya mara kwa mara, na wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakilalamikia alama duni za barabarani, kwa mujibu wa AEA club.

Ripoti ya La Opinion de Zamora inaeleza kuwa malalamiko 40 ya mashimo barabarani yaliwasilishwa kwa Wizara ya Uchukuzi ya Hispania kwa mwezi mmoja tu mwaka 2024.

Eneo la Zamora pia linajulikana kwa kuwa na ardhi yenye milima na misitu, barabara ya A-52 ikipita katikati ya maeneo hayo, yenye ukungu wa mara kwa mara na mwanga hafifu usiku.