Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rio Ferdinand kasema... Man United inashuka

Muktasari:

  • Gwiji huyo wa Old Trafford hana tena imani na kikosi hicho cha Kocha Ruben Amorim ambacho bado kipo kwenye michuano ya Europa League na Kombe la FA, lakini hali ni mbaya Ligi Kuu England, kikiwa na pointi 12 tu juu ya timu zilizo kwenye kundi la kushuka daraja.

LONDON, ENGLAND: RIO Ferdinand amefichua wasiwasi wake huenda Manchester United isipate ushindi wowote tena kwenye mechi zilizobaki kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Gwiji huyo wa Old Trafford hana tena imani na kikosi hicho cha Kocha Ruben Amorim ambacho bado kipo kwenye michuano ya Europa League na Kombe la FA, lakini hali ni mbaya Ligi Kuu England, kikiwa na pointi 12 tu juu ya timu zilizo kwenye kundi la kushuka daraja.

Kwa kifupi, beki wa kati huyo wa zamani amebainisha wasiwasi wake juu ya kuiona Man United ikishuka daraja na kwenda kucheza kwenye Championship msimu ujao.

Man United kwa sasa inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi baada ya kupoteza mechi 12 msimu huu kutokana na kichapo cha bao 1-0 huku ikicheza kwa kiwango kibovu kabisa dhidi ya Tottenham.

Vipigo 12 ni vingi sana kwenye mechi zao 25 za kwanza kwenye ligi tangu msimu wa 1973-74 - ambao uliishuhudia timu hiyo ikishuka daraja.

Ferdinand, 46, alisema kupitia chaneli yake ya YouTube: “Ni Wolves na West Ham tu ndizo zilizoitenganisha klabu yangu kutoka kwenye nafasi za kushuka daraja. Unaweza kuona jinsi tulivyokaribu. Kuna mtu amesema tunahitaji pointi 11 kubaki kwenye ligi.

“Nimetazama ratiba: Everton ugenini, Ipswich nyumbani, Arsenal na Nottingham Forest ugenini. Kabla ya kuwakaribisha Man City, na kuwafuata Newcastle, kisha Wolves, Bournemouth, Brentford, Chelsea, Aston Villa, Leicester. Sehemu pekee ambayo naona tunaweza kupata chochote na sisemi ni ushindi ni Leicester. Sioni ushindi. Hilo ndio tatizo.”€

Mwezi mmoja uliopita, Everton ilikuwa nyuma kwa pointi tisa dhidi ya Man United, lakini sasa imepanda juu pointi moja kwenye msimamo wa ligi baada ya kumchukua kocha David Moyes.

Ferdinand hofu imezidi zaidi baada ya Man United kukutana na vichapo vinane chini ya kocha Amorim, ambaye alijiunga na klabu hiyo Novemba mwaka jana.

Ushindi kwenye mechi chache tu utabadili kila kitu na kuirudisha Man United kwenye msimamo na kuondoa hofu ya kushuka daraja huku ikipambana pia kwenye Kombe la FA na Europa League.

Kwa sasa Man United ina pointi 29 katika mechi 25, pointi 31 nyuma ya vinara Liverpool.