Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rekodi za Amorim zashtua Man United

Muktasari:

  • Kocha Amorim ameshindwa kubadili hali ya mambo kwenye timu hiyo, ambapo Jumapili iliyopita Man United ilichapwa na Tottenham, hivyo ikishuka hadi kwenye nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi.

MANCHESTER, ENGLAND: HAKUNA kocha wa Manchester United aliyevuna pointi chache kumzidi Ruben Amorim baada ya mechi 14 za Ligi Kuu England tangu Sir Alex Ferguson alipong'atuka kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.

Kocha Amorim ameshindwa kubadili hali ya mambo kwenye timu hiyo, ambapo Jumapili iliyopita Man United ilichapwa na Tottenham, hivyo ikishuka hadi kwenye nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi.

Kinachoonekana ni kwamba Amorim bado hajapata njia sahihi ya kikosi hicho kucheza, ambapo akianza maisha yake ya Old Trafford kwa sare mbele ya Ipswich Town na baadaye kushinda dhidi ya Everton kwenye mechi ya pili, kocha huyo Mreno ameshuhudia akipoteza mechi nane kati ya 12 zilizofuatia.

Ndani ya muda huo ilifanikiwa pia kuzishinda Manchester City, Southampton na Fulham, lakini pointi ilizokusanya Man United kwenye mechi hizo 14 ni chache kuliko zilizowahi kuvunwa na watangulizi wake.

Kwa wastani wa kuvuna pointi moja kwa kila mechi inamfanya Amorim kuwa kwenye hatari ya kufikisha pointi 50. Msimu uliopita, Erik ten Hag alikuwa na wakati mgumu, lakini Mdachi huyo kwenye mechi zake 14 za kwanza kwenye kikosi hicho cha Man United alivuna pointi za kutosha, si kama sasa ilivyo kwa Amorim.

Baada ya mechi 14 kwenye Ligi Kuu England, pointi zinazofuatia kwa uchache ambazo zilivunwa baada ya Ferguson kung'atuka 2013, ni zile zilizovunwa na Jose Mourinho, pointi 21, ambapo msimu huu alienda kumaliza nafasi ya sita katika msimamo wa ligi hiyo.

David Moyes, ambaye ndiye aliyerithi mikoba ya Ferguson, hakuwa na wakati mzuri kwenye kikosi hicho na kuondoka kabla ya msimu kumalizika, lakini kwenye mechi 14 za kwanza alivuna pointi nyingi kumzidi Amorim, ambapo Mskochi huyo alinyakua pointi 22.


POINTI ZILIZOVUNWA NA MAKOCHA WA MAN U KATIKA MECHI 14 ZA KWANZA KWENYE EPL.

1.Solskjaer - pointi 35

2.Rangnick - pointi 26

2.Ten Hag - pointi  26

4.Van Gaal - pointi 25

5.Moyes - pointi 22

6.Mourinho - pointi 21

7.Amorim - pointi 14