Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Reece, dada’ke ‘kuzeekea’ Chelsea

Muktasari:

  • Sambamba na Reece, dada yake, Lauren naye amesaini mkataba mpya utakaomfanya kuichezea timu hiyo ya wanawake miaka sita zaidi.

LONDON, ENGLAND: NAHODHA wa Chelsea, Reece James ameahidi kubaki muda mrefu zaidi baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka sita utakaomuweka Stamford Bridge hadi 2032, ambapo atakuwa na umri wa miaka 32.

Sambamba na Reece, dada yake, Lauren naye amesaini mkataba mpya utakaomfanya kuichezea timu hiyo ya wanawake miaka sita zaidi.

Reece, mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika 2028, lakini inaaminika kuwa beki huyo mwenye miaka 26, ambaye ni zao la akademi ya klabu hiyo amekubaliana na masharti mapya yanayoendana na mfumo wa mishahara wa Chelsea.

Mashabiki wa Chelsea wamepokea habari hizo kwa furaha kwani nahodha ameahidi kutumia miaka yake bora ya soka katika klabu hiyo. Hadi sasa, Reece ameichezea Chelsea mechi 225 katika mashindano yote.

Daily Mail inaripoti kuwa mazungumzo ya mkataba wa nyota huyo yalikuwa yamefikia hatua muhimu na kwamba  wamiliki wa Chelsea hawataki wachezaji wao mahiri kufika miaka miwili ya mwisho ya mikataba yao bila kuiongeza, hasa baada ya kuwapoteza Antonio Rudiger na Andreas Christensen bure walipojiunga na Real Madrid na Barcelona baada ya wamiliki wapya klabuni kutua 2022.

Lakini, sasa imethibitishwa Reece atabaki Chelsea kama sehemu ya kutambua maendeleo yake akiwa  kiongozi ndani ya kikosi. Tayari nyota huyo ameshinda mataji kadhaa akiwa Chelsea, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya 2021.

Kwa sasa ndiye mchezaji pekee aliyebaki klabuni kutoka kikosi kilichoshinda taji hilo wakati wa umiliki wa Roman Abramovich. Pia anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha England kinachofundishwa na Thomas Tuchel katika Kombe la Dunia litakalofanyika Amerika, Juni, mwaka huu.


LAUREN APEWA DILI JIPYA

Mshambuliaji wa Chelsea wanawake, Lauren ambaye wanafuatana na Reece, naye amesaini mkataba mpya utakaomweka Chelsea hadi 2030.

Mchezaji huyo mwenye miaka 24 alianzia katika akademi ya Chelsea kabla ya kuondoka kisha kurejea 2021 akitokea Man United. Tangu arejee Lauren amefunga mabao 31 katika mechi 105 alizoichezea Chelsea na kuwa mmoja wa wachezaji muhimu licha ya kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

Akizungumzia dili lake, Lauren alisema: “Nina furaha sana kusaini mkataba mpya na Chelsea. Hii imekuwa klabu yangu tangu nilipokuwa mdogo. Natarajia kutengeneza kumbukumbu zaidi, kupata mafanikio na kushinda mataji mengi zaidi.”