Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bei anayouzwa Rashford imetajwa

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Aston Villa imewekewa kipengele hicho cha kumchukua staa huyo wa Man United baada ya kumalizia nusu ya pili ya msimu huu kwenye kikosi chao akicheza kwa mkopo.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imetaja bei anayouzwa winga Marcus Rashford na timu itakayohitaji huduma ya staa huyo dirisha lijalo la usajili itapaswa kulipa Pauni 40 milioni.

Aston Villa imewekewa kipengele hicho cha kumchukua staa huyo wa Man United baada ya kumalizia nusu ya pili ya msimu huu kwenye kikosi chao akicheza kwa mkopo.

Hata hivyo, Aston Villa inayonolewa na Mhispaniola Unai Emery haijamweka Rashford kwenye mpango wao mkuu wa kumsajili na badala yake milango ipo wazi kwa timu nyingine zinazomtaka kumsajili.

Rashford baada ya kushindwa kuikabili Tottenham usiku wa Ijumaa, hiyo ina maana hataonekana tena kwenye uzi wa Aston Villa msimu huu kwa sababu mechi ya mwisho wa msimu itakipiga na Man United, timu yake hivyo hataruhusiwa kucheza.

Na kama hakutakuwa na timu nyingine inayomtaka, Rashford atalazimika kurejea Carrington kwa ajili ya pre-season mapema Julai.

Lakini, haionekani kama atakuwa na maisha ya kuichezea klabu yake hiyo tangu enzi za utoto kama kocha Ruben Amorim ataendelea kubaki Old Trafford. Ishu inayowakabili Man United ni kutafuta timu itakayokuwa tayari kumlipa Rashford Pauni 315,000 kwa wiki kwa sababu hataki kupunguza mshahara.

Aston Villa inaripotiwa ilikuwa inalipa asilimia 75 ya mshahara wa mchezaji huyo alipokuwa Villa Park kwa muda wake wa mkopo huo. Sasa mpango wa kumtoa tena kwa mkopo kama itashindwa kumbeba jumla huo unaweza kufanyika.

Rashford aliweka wazi anataka kujiunga na timu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Alirudishwa kwenye kikosi cha England baada ya kufanya vizuri Aston Villa, ambako alifunga mabao manne na kuasisti mara sita katika mechi 18 alizocheza na miamba hiyo kabla ya kuwa majeruhi siku za karibuni.