Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford Barcelona ndo basi tena

Muktasari:

  • Nguvu ya matumizi ya klabu hiyo ya Catalonia imepunguzwa kwa takribani Pauni 100 milioni kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa hivi karibuni.

BARCELONA, ENGLAND: MATUMAINI ya Marcus Rashford ya kufanya uhamisho wake wa mkopo kwenda Barcelona kuwa wa kudumu yamefifia kutokana na vizuizi vipya vya mishahara vilivyowekwa na LaLiga.

Nguvu ya matumizi ya klabu hiyo ya Catalonia imepunguzwa kwa takribani Pauni 100 milioni kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa hivi karibuni.

Mchezaji huyo anayeichezea Barca kwa mkopo kutoka Manchester United ameanza maisha yake Hispania kwa kishindo, akifunga mabao mawili aliporejea England kwenye ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Newcastle United wiki hii.

Lakini licha ya kiwango hicho cha juu, mabingwa hao wa Hispania sasa wanalazimika kufanya kazi katika kiwango kipya cha mishahara kilichopunguzwa ili kumsainisha mkataba wa kudumu au hata kusajili wachezaji wengine dirisha lijalo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania, LaLiga ilitangaza Ijumaa kiwango cha mishahara rasmi cha Barcelona kwa msimu wa 2025-26 kimepunguzwa kutoka Euro 463 milioni hadi Euro 351 milioni, ambayo ni pungufu wa Euro 112 milioni.

Kiwango hiki kinaonyesha kiwango cha juu ambacho kila klabu inaweza kutumia kwenye mishahara na gharama nyingine za kikosi. Ikiwa timu itazidisha kiwango hicho, LaLiga haitoruhusu wachezaji wapya kuingizwa katika mfumo wa usajili ili  kushiriki katika mashindano rasmi.

Inadaiwa kupunguzwa huko kunahusishwa na utata wa kifedha kuhusiana na mapato ya VIP kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Wakaguzi wa awali wa hesabu za klabu walihesabu Euro 100 milioni zilizopatikana kutokana na kuuza tiketi za VIP kwa muda wa miaka 25 ijayo kama sehemu ya mapato.

Hata hivyo, wakaguzi wa sasa wamekataa kuthibitisha fedha hizo kama mapato, jambo ambalo limesababisha zisihesabiwe katika makadirio ya mishahara.

Kuhama kwa Barcelona kutoka Camp Nou kwa sababu ya kupisha ukarabati pia inadaiwa kuathiri mapato yao.

Mabingwa hao watetezi wa La Liga Wamelazimika kucheza mechi za nyumbani kwenye viwanja vya muda mfupi, ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Johan Cruyff wenye uwezo wa watazamaji 6,000, wakati Nou Camp ukiendelea kufanyiwa ukarabati wa Pauni 1.2 bilioni.

Viongozi wakuu wa LaLiga wamesema kupungua kwa mapato ya viingilio vya uwanjani kumeathiri vibaya uwezo wa klabu hiyo kufanya usajili mkubwa.

Kwa mujibu wa The Athletic, Barcelona imesisitiza haina tatizo na kiwango kipya cha mishahara.

Wanaamini kurejea Camp Nou kutasaidia kurekebisha hali hiyo kwa kuongeza mapato ya mechi na kurejesha Euro 100 milioni iliyokataliwa kutambulika kama mapato.