Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford alilia mchongo wa Barcelona

Muktasari:

  • Rashford ambaye alijiunga na Aston Villa kwa mkopo wa nusu msimu, mkataba wake na Man United unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, kwa sasa anapokea mshahara unaokadiriwa kufikia Pauni 300,000 kwa wiki.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Marcus Rashford yuko tayari kukubali kupunguziwa mshahara ili kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi na kujiunga na Barcelona inayodaiwa kumhitaji.

Rashford ambaye alijiunga na Aston Villa kwa mkopo wa nusu msimu, mkataba wake na Man United unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, kwa sasa anapokea mshahara unaokadiriwa kufikia Pauni 300,000 kwa wiki.

Barcelona imekuwa ikihusishwa na fundi huyu mara kadhaa hapo awali lakini changamoto kubwa imekuwa ni kiasi cha pesa ambacho Man United ilikuwa inahitaji ili kumuuza.

Akiwa na Villa kwa mkopo Rashford alionyesha kiwango bora kilichozivutia timu nyingi na hataki tena kurudi Man United kwa sababu haoni kama atapata nafasi ya kucheza mbele ya Rubem Amorim aliyesema mara kadhaa kwamba haridhishwi na utendaji kazi wake.


Morgan Rogers

CHELSEA imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa, Morgan Rogers, mwenye umri wa miaka 22, ikiwa ni katika harakati za kuboresha eneo la ushambuliaji.

Mkataba wa sasa wa Morgan unatarajiwa kumalizika mwaka 2030. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 50 za michuano yote, amefunga mabao 14 na kutoa asisti 13.


Dean Huijsen


LIVERPOOL inataka kuwasajili mabeki wa Bournemouth, Dean Huijsen, 20 na Milos Kerkez, 21, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi pamoja na mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, 22.

 Mabosi wa Liverpool inataka kusajili washambuliaji hawa kwa ajli ya kuboresha kikosi na kutetea taji lake la EPL msimu ujao.


Sandro Tonali


KIUNGO wa kati wa Italia, Sandro Tonali, anapanga kubaki Newcastle United kwa muda mrefu, licha ya kuhusishwa na timu mbalimbali za Italia.

Tonali ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu huu amecheza mechi 41 za michuano yote na kufunga mabao matano.


Jack Grealish

MANCHESTER City haina mpango wa kumruhusu kiungo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 29, Jack Grealish, kuondoka katika dirisha hili licha ya tetesi zinazodai kwamba anaweza kutua Bayern Munich.

Grealish ni miongoni mwa wachezaji ambao hawapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Man City hali inayosababisha kuwepo kwa tetesi za kuondoka kwake.


Joan Garcia

MABOSI wa Aston Villa wapo tayari kulipa Pauni 21 milioni kwenda Espanyol kwa ajili ya kuipata saini ya kipa wa timu hiyo na Hispania, Joan Garcia, mwenye umri wa miaka 23.

Garcia ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, anawindwa na timu nyingi barani Ulaya kutokana na kiwango alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu.


Andrea Cambiaso

LIVERPOOL na Manchester City  ni miongoni mwa timu zinazovutiwa na beki wa kulia wa Juventus na timu ya taifa ya  Italia, Andrea Cambiaso 25, ambaye anaonekana kuwa karibu kuondoka  katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Vigogo wa Liverpool ndio wanaonekana kuwekeza nguvu zaidi katika dili la fundi huyu kwa sababu hawana uhakika ikiwa Trent Alexander Arnold.


Rayan Cherki

MANCHESTER United na Tottenham zipo katika vita kali ya kuiwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Olympique Lyon na timu ya taifa ya Ufaransa, Rayan Cherki, mwenye umri wa miaka 21. Vigogo hawa wamevutiwa sana na Cherki kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu msimu uliopita ambapo alicheza mechi 41 na kufunga mabao 12.