Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lehmann: Arteta atafutwa kazi

LEHMAN Pict

Muktasari:

  • Arsenal inaelekea kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya Liverpool kutangazwa kuwa mabingwa wa msimu huu, Jumapili iliyopita.

LONDON, ENGLAND: GWIJI wa Arsenal, Jens Lehmann amesema kocha wa sasa wa timu hiyo Mikel Arteta atajiweka kwenye hatari ya kufutwa kazi endapo atashindwa kubeba taji la Ligi Kuu England msimu ujao.

Arsenal inaelekea kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya Liverpool kutangazwa kuwa mabingwa wa msimu huu, Jumapili iliyopita.

Ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Tottenham uliifanya Liverpool kushinda taji la 20 la Ligi Kuu baada ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Arne Slot kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 15 na bado kuna mechi nne msimu kufika tamati.

Arsenal ilishindwa kuchuana na Liverpool kwenye mzunguko wa pili wa ligi, lakini imekuwa na kiwango kizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na iliisukuma nje Real Madrid kwa jumla ya mabao 5-1 kwenye robo fainali na kukabiliana na Paris Saint-Germain katika mchezo wa nusu fainali.

Licha ya kutengeneza nafasi nyingi, Arsenal ilipoteza mechi ya kwanza 1-0, shukrani kwa bao la Mfaransa, Ousmane Dembele na hivyo kusubiri mechi ya marudiano itakayopigwa Jumatano ijayo.

Bado kuna nafasi Arsenal inaweza kutinga fainali na kunyakua kombe msimu huu, lakini Lehmann anaamini Arteta amejiweka kwenye wakati mgumu wa kufutwa kazi msimu ujao labda kama tu atafanikiwa kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England.

Lehmann alisema: “Nadhani alianza vibaya, lakini kwa sasa sifa zote zielekezwe kwake. Amejipambanua, amebadilisha timu na sasa imekuwa imara na inacheza vizuri na mabosi wapo vizuri, wanampa pesa. Kutokana na hilo, kama atashindwa kubeba ubingwa, hakutakuwa na kitu cha ziada kwake.”

Lehmann aliongeza: “Ni lazima ashinde kitu mwakani. Msimu huu angeweza kushinda Ligi Kuu England. Man City ilishuka, lakini Liverpool imekuja kuchukua nafasi. Mwakani ni lazima ashinde, akishindwa basi kuna shida inaweza kumkukuta.”