Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Raphinha nusura aipige kibuti FC Barcelona

RAPHINHA Pict

Muktasari:

  • Raphinha hakuwa na msimu mzuri sana 2023-24 kwenye kikosi cha Barcelona, ambako alifunga mabao 10 na kuasisti 13 katika mechi 37 alizocheza kwenye michuano yote na hilo lilisababisha kuibuka kwa uvumi mwingi wa kuhusu hatima yake hiyo mwaka jana.

BARCELONA, HISPANIA: STAA wa Kibrazili, Raphinha amefichua kwamba nusura aachane na Barcelona msimu uliopita, lakini ujio wa kocha Mjerumani Hansi Flick ulimbadili mawazo na kubaki Camp Nou.

Raphinha hakuwa na msimu mzuri sana 2023-24 kwenye kikosi cha Barcelona, ambako alifunga mabao 10 na kuasisti 13 katika mechi 37 alizocheza kwenye michuano yote na hilo lilisababisha kuibuka kwa uvumi mwingi wa kuhusu hatima yake hiyo mwaka jana.

Na hilo lilimfanya Raphinha, 28, mwenyewe kufikiria kuondoka hadi hapo alipozungumza na kocha Flick aliyemshawishi kubaki Nou Camp hadi msimu huu.

"Nilikuwa nafikiria kuondoka Barcelona baada ya Copa America kwa sababu sikuwa nikipata utulivu wa kisaikolojia hadi hapo Flick aliponipigia," alisema Raphinha.

"Kile kipindi kilikuwa kigumu sana. Kila siku ulikuwa unasikia habari kwamba nakwenda kujiunga na timu hii na ile. Nilikuwa na msimu mbaya na watu walitaka niondoke."

Raphinha amekuwa mmoja wa wachezaji mahiri sana msimu huu, akifunga mabao 27 na kuasisti mara 20 katika mechi 42 za michuano yote.

Mbrazili huyo amefunga mara 13 na asisti 10 kwenye mechi 27 za La Liga, lakini kiwango chake kimekuwa bora pia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambako amefunga mabao 11 na asisti tano katika mechi 10 alizocheza katika michuano hiyo msimu huu.

"Ukweli, Ballon d'Or sio malengo yangu binafsi," alisema juu ya tuzo hiyo na kuongeza. "Malengo yangu ni kufunga mabao, kuasisti na kuisaidia Barcelona na timu ya taifa kushinda mataji. Mambo yanapokuwa mazuri kwa klabu na timu ya taifa basi hata kiwango chako binafsi kinakuwa vizuri."