Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Raphinha katika rada za Manchester United

TETESI Pict

Muktasari:

  • Raphinha mwenye umri wa miaka 28, kwa sasa ni mmoja kati ya mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Barca na msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao 27.

MANCHESTER United imewasilisha ofa ya Euro 70 milioni kwenda Barcelona kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Brazil, Raphinha, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Raphinha mwenye umri wa miaka 28, kwa sasa ni mmoja kati ya mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Barca na msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao 27.

Kocha wa Man United, Ruben Amorim anahitaji kusajiliwa kwa Raphinha kwa sababu anaamini ni moja kati ya majibu sahihi ya kuondoa ubutu kwenye eneo lao la ushambuliaji.

Hata hivyo, dili hili linaonekana litakuwa gumu ikiwa Man United itashindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa, michuano ambayo anataka kucheza.


Victor Osimhen

BEKI wa kati wa Al Kholod na timu ya taifa ya Nigera, William Troost-Ekong ameweka wazi kwamba mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ambaye ni mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen, mwenye umri wa miaka 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo  Galatasaray, anatarajia kujiunga na timu ya Ligi Kuu England kwa msimu ujao. Osimhen ambaye mkataba wake na Napoli unamalizika mwaka 2026, akiwa na Galatasaray msimu huu amecheza mechi 30 za michuano yote na kufunga mabao 26.


Eduardo Camavinga

MANCHESTER City imeambiwa kuwa itatakiwa kulipa walau Pauni 70 milioni ili kuipata huduma ya kiungo wa Real Madrid na Ufaransa, Eduardo Camavinga, 22, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Camavinga ambaye amekuwa akihusishwa na Chelsea ambayo ipo tayari kumtumia Enzo Fernandez kama sehemu ya ofa ya kumpata, mkataba wake unamalizika mwaka 2029. Staa huyo amekuwa akichezeshwa kama beki wakati mwingine.


Marcus Thuram

ARSENAL na Chelsea zimetumbukia katika vita dhidi ya Liverpool kwa ajili ya kuipata saini ya mshambuliaji wa Inter Milan na Ufaransa, Marcus Thuram, 27. Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya Football Insider, katika mkataba wa Thuram inaelezwa kuwa kipengele ambacho kinamruhusu kujiunga na timu yoyote anayohitaji ni ada ya Pauni 71 milioni. Msimu huu amecheza mechi 38 za michuano yote na kufunga mabao 16.


Benjamin Cremaschi

TOTTENHAM Hotspur ni miongoni mwa timu kadhaa kutoka Ligi Kuu England ambazo zinahitaji saini ya kiungo wa Inter Miami na Marekani, Benjamin Cremaschi, 20, katika dirisha lijalo.

Licha ya kuhitajika na timu nyingi za England, Benjamin sio mmoja kati ya mastaa wanaopata nafasi kubwa ya kucheza kwenye kikosi cha Miami na msimu huu amecheza mechi nane za michuano yote. Mkataba wake unamalizika mwaka 2027.


Jorrel Hato

ARSENAL imepanga kumchukua beki wa kushoto wa Ajax na Uholanzi, Jorrel Hato, 19, licha ya uwepo wa beki kinda Myles Lewis-Skelly anayeweza kucheza eneo hilo.

Ripoti zinaeleza Arteta amependekeza kusajiliwa kwa Hato kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza nafasi zaidi ya moja kwani mbali ya kuwa beki wa kushoto pia anatumika kama beki wa kati.


Alexander Isak

NEWCASTLE inataka kufanya kila linalowezekana kumbakisha mshambuliaji wao raia wa Sweden, Alexander Isak, lakini ikiwa itashindwa kufanya hivyo, imepanga kusajili mbadala wake ambaye anaweza kuwa straika wa Ipswich Town, Liam Delap, mwenye umri wa miaka 22, na straika wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres, 26.


Christian Pulisic

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea na Marekani, Christian Pulisic, 26, yuko kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na  mabosi wa AC Milan.

Vigogo wa Milan wanataka kumsainisha mkataba mpya Pulisic kutokana na mchango wake mkubwa aliouonyesha kwa karibia misimu miwili. Msimu huu amefunga mabao 15.