Promota afichua kilichomponza Joshua

APRILI Mosi, bondia Anthony Joshua anatarajiwa kupanda ulingoni kurudisha ubabe wake wa ushindi mbele ya bondia Jermaine Franklin katika pambano litakalofanyika ukumbi wa 02 Arena jijini London nchini England.

Hilo litakuwa pambano mahsusi kwa Joshua maarufu kama AJ ambaye mara ya mwisho alipoteana dhidi ya bondia Oleksandr Usyk katika mapambano mawili mtawalia yaliyofanyika mwaka jana nchini Saudia na England.

Ili kumrudishia umwamba wake, AJ amelazimika kubadilisha wakufunzi wake mara tatu ndani ya miaka mitatu na safari hii akikutana na mkufunzi Derrick James ambaye anaelezwa kambadilisha kwa ukubwa Joshua.

Promota Eddie Hearn amefichua kuwa kwenda kwake kwenye mazoezi ya Joshua ndani ya ‘gym’ ya James amekuwa akimkuta AJ amechoka sana tofauti na ilivyowahi kuwa kabla jambo linalomaanisha kwamba, awali alikuwa anafanyishwa mazoezi kwa hofu ya kutomchosha kisa jina lake liko juu katika masumbwi.