Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Potter afungashiwa virago West Ham

Muktasari:

  • Potter amefukuzwa na timu hiyo kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo ambao wamekuwa wakiyapata tangu kuanza kwa msimu huu.

LONDON, ENGLAND: KOCHA Graham Potter ametimuliwa na West Ham United saa chache zilizopita, licha ya kuongoza mazoezi kwa wiki nzima kuelekea mechi za wikiendi hii.

Potter amefukuzwa na timu hiyo kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo ambao wamekuwa wakiyapata tangu kuanza kwa msimu huu.

West Ham ilipokea kichapo cha mabao 2-1, kutoka kwa Crystal Palace Jumamosi iliyopita ambacho kilikuwa ni kipigo chao cha tatu mfululizo kwenye Uwanja wao wa nyumbani tangu kuanza kwa msimu huu.

Vilevile hiyo ilikuwa ni mechi yao ya nne kufungwa katika Ligi Kuu England kwa msimu huu ambapo hadi sasa ina pointi tatu tu na inashika nafasi ya 19.

Katika taarifa iliyowekwa katika tovuti na kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ilisema: "West Ham United inathibitisha kwamba Kocha Mkuu Graham Potter ameondoka klabuni. Matokeo mabovu na kiwango cha timu katika nusu ya pili ya msimu uliopita na mwanzoni mwa msimu wa 2025/26 hayakuwa yanalingana na matarajio yetu, hivyo Bodi ya Wakurugenzi inaamini kuwa mabadiliko ni muhimu ili kuiboresha timu na kuiweka katika mstari.

"Vilevile makocha wasaidizi Bruno Saltor, Billy Reid na Narcis Pelach na kocha mkuu wa makipa Casper Ankergren, msaidizi  wake Linus Kandolin nao pia tumeachana nao.

"Bodi inamshukuru Graham na benchi lake la ufundi kwa kazi ngumu na kubwa waliyoifanya wakiwa hapa. Mchakato wa kumpata mbadala wake unaendelea."

Wiki iliyopita wakati mchezo wa Crystal Palace ukiendelea mashabiki walikuwa wakiimba kutaka kocha huyo aondolewe kwa sababu waliona amefeli.

Kocha wa zamani wa timu hiyo, Slaven Bilic anahusishwa kuwa katika mchakato wa kurejeshwa na pia Nuno Espirito Santo na Gary O’Neil wanatajwa tajwa.

Potter alijiunga na West Ham United, Januari, mwaka huu, akichukua nafasi ya Julen Lopetegui na tangu wakati huo ameongoza timu hiyo kushinda mechi sita kati ya 25.