Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pogba ruksa kukipiga tena

POGBA Pict

Muktasari:

  • Mwanzoni Pogba alifungiwa soka miaka minne baada ya kupimwa na kugundulika kuwa alitumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, jambo lililomfanya akate rufaa kwenye mahakama ya rufani michezoni (CAS) kupinga adhabu hiyo na kupunguziwa hadi miezi 18, ambayo iliishia Machi 11, 2025.

PARIS, UFARANSA: JUMANNE, Machi 11 ilikuwa siku ya mwisho kwa kiungo Mfaransa Paul Pogba kutumikia adhabu ya kufungiwa soka na sasa, mkali huyo wa zamani wa Manchester United na Juventus yupo huru kukipiga tena kuanzia Jumatano, Machi 12, 2025.

Mwanzoni Pogba alifungiwa soka miaka minne baada ya kupimwa na kugundulika kuwa alitumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, jambo lililomfanya akate rufaa kwenye mahakama ya rufani michezoni (CAS) kupinga adhabu hiyo na kupunguziwa hadi miezi 18, ambayo iliishia Machi 11, 2025.

Sasa Pogba yupo huru kurudi kwenye soka la kulipwa akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake Juventus, Novemba 15, mwaka jana. Hata hivyo, kurudi kwenye klabu kubwa au huko kwenye Serie A ni jambo gumu kutokana na kelele za vyombo vya habari huku akiwa hajacheza mechi yoyote ya kiushindani kwa muda mrefu. Eneo pekee Pogba analoweza kuibukia kwa sasa ni Ligi Kuu Marekani (MLS) au kwenye Saudi Pro League huko Saudi Arabia.