Pogba arudi uwanjani Monaco ikilala ugenini
Muktasari:
- Miezi mingi ya kusubiri, tetesi zisizoisha na mazungumzo ya kisiri hatimaye yalifika mwisho.
Uwanja wa Stade Louis II ulifurika watazamaji kuliko ilivyozoeleka. Wapenzi wa soka walikuwa wamebeba mabango mekundu na meupe, wengine wakiwa na jina moja tu lililoangaza juu yao, POGBA.
Miezi mingi ya kusubiri, tetesi zisizoisha na mazungumzo ya kisiri hatimaye yalifika mwisho.
Mizunguko ya kamera ilihama ghafla iliposikika kelele kutoka katika sehemu ya kuingia wachezaji.
Mlango ukafunguka taratibu na hapo, kwa hatua zake zinazotambulika, Paul Labile Pogba akaonekana.
Sio tu kama mchezaji, bali kama mtu aliyepitia majaribu na kurejea akiwa imara kuliko awali.
Jezi mpya ya AS Monaco, namba 6 mgongoni ilimkaa kama hadithi iliyokuwa ikisubiri kuandikwa upya.
Mashabiki wakaanza kuimba: “Pogba! Pogba! Pogba!”
Kwa muda mfupi, kelele zote zilitoweka kichwani mwake, alifika katikati ya uwanja akaangalia majukwaa, kisha akapumua.
Hakukuwa tena na mzigo wa shinikizo ni upendo, furaha na ari ya kuonyesha kwamba safari ya mchezaji haimalizwi na changamoto.
Mechi ya Ligue 1 ilipoanza, Monaco ilionesha kasi, lakini macho ya wengi yalikuwa kwa Pogba aliyeanzia benchi.
Dakika tano kabla ya filimbi ya mwisho, Pobga aliingizwa uwanjani na mpira ulipomfikia mara ya kwanza, aliugeuza kwa ustadi ule ule uliozoeleka ‘first touch maridadi’, kisha pasi ndefu iliyovunja mstari wa kiungo wa wapinzani.
Uwanja mzima ukalipuka kwa makofi.
Kadri dakika zilivyozidi kusonga, Pogba alionyesha kila kitu kilichomfanya awe mchezaji mashuhuri duniani: Ubunifu, guvu, utulivu na tabasamu lake la kipekee alipoweka pasi ya mwisho kwa mshambuliaji wao mchanga aliyefunga goli kwa ueledi.
Kocha wa Monaco alisimama tu pembeni, akitabasamu kama mtu aliyepata hazina aliyokuwa akiitamani kwa muda mrefu.
Wakati kipenga cha mwisho kilipopulizwa, mashabiki waliimba jina lake tena. Pogba hakutabasamu tu, alikumbwa na hisia, aliangaliwa juu, mikono hewani, akihisi kwamba alikuwa amerejea si tu kama mchezaji, bali kama mshindi aliyeandika sura mpya ya maisha yake.
Na siku hiyo, katika jiji dogo lenye historia kubwa ya michezo, kulizaliwa hadithi mpya: Paul Pogba, Mfalme Mpya wa Monaco.
Katika mechi hiyo iliyopigwa jana Jumamosi, Monaco ikiwa ugenini iliichapwa na wenyeji Rennes kwa mabao 4-1, huku ikimaliza pungufu baada ya Dennis Zakaria kulimwa kadi nyekundu dakika ya 66.
Pogba aliingia uwanjani dakika ya 85 kumpokea Mamadou Coulibaly.