Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pogba, Monaco mambo yanazidi kuwa magumu

Muktasari:

  • Kibarua cha kocha Adi Hutter kipo kwenye mashaka makubwa licha ya kuisaidia timu hiyo kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

MONACO, UFARANSA: KIUNGO Paul Pogba bado hajacheza mechi yoyote kwenye klabu yake mpya huko AS Monaoc, lakini huenda asipate kabisa nafasi ya kucheza chini ya kocha aliyemnunua huko Stade Louis II.

Kibarua cha kocha Adi Hutter kipo kwenye mashaka makubwa licha ya kuisaidia timu hiyo kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Kocha huyo Muastria, Hutter ameanza msimu kwa kushinda mechi nne kati ya tano, huku mchezaji mwenzake Pogba, waliyesajiliwa pamoja Ansu Fati akionyesha kiwango bora kabisa.

Lakini, mambo yamegeuka, baada ya kuchapwa 4-1 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Club Brugge, Monaco ilishindwa kupata ushindi kwenye mechi mbili zilizofuata dhidi ya Ligue 1.

Kwa mujibu wa L’Equipe, Monaco inafikiria kumbadili kocha huyo. Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Edin Terzic ni miongoni mwa wanaosakwa na timu hiyo baada ya kuachana na klabu hiyo ya Bundesliga, ambayo alifika nayo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2024.

Baada ya kipigo kutoka kwa Lorient mwishoni mwa Septemba, Monaco ya Hutter iliambulia sare dhidi ya Manchester City kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ilishindwa kupata ushindi kwenye mechi ya ligi iliyofuata baada ya kutoka sare na Nice.

Bado hatujapata suluhisho katika sehemu ya ushambuliaji,” alisema Hutter baada ya sare ya 2-2 Jumapili iliyopita.

“Sijaridhika kwa asilimia 100. Hatujarahi. Wachezaji watakaporudi, tutakuwa kwenye ubora.”

Pogba alikuwa na matumaini ya kuanza kuichezea timu yake ya Monaco wikiendi hii kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Angers, lakini alipata maumivu mengine mazoezini.