Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pigo City, Gvardiol avunjika mguu

PIGO Pict

Muktasari:

  • Jeraha hilo linaweza kumlazimu Pep Guardiola na benchi la ufundi kuanza harakati za kumsajili beki wa England, Marc Guehi.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City imethibitisha beki kisiki, Josko Gvardiol amevunjika mguu.

Jeraha hilo linaweza kumlazimu Pep Guardiola na benchi la ufundi kuanza harakati za kumsajili beki wa England, Marc Guehi.

Gvardiol, 23, alitolewa nje katika dakika ya 51 ya mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea siku ya Jumapili, baada ya kugongana vibaya na mchezaji mwenzake.

Beki huyo aliweza kutembea kwa kujikongoja bila kutumia machela, akisaidiwa na nahodha wa Chelsea, Reece James.

Hofu za awali kuhusu hali ya Gvardiol sasa zimethibitishwa, huku mchezaji huyo wa Croatia akitarajiwa kufanyiwa upasuaji.

Taarifa ya klabu ilisema: “Manchester City FC inathibitisha kuwa Josko Gvardiol amepata tatizo la mfupa wa tibia kuvunjika kwenye mguu wake wa kulia.

“Jeraha hilo lilitokea katika kipindi cha pili cha sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea kwenye Ligi Kuu England, Jumapili.

PIG 01
PIG 01

“Beki huyo atafanyiwa upasuaji baadaye wiki hii, na tathmini bado inaendelea ili kubaini ukubwa kamili wa jeraha na muda wa kupona.”

Gvardiol pia alielezea masikitiko yake kupitia akaunti za Instagram na X (Twitter).

Aliandika: “Huu ni wakati mgumu, lakini hautanivuruga kamwe. Najua mimi ni nani na ninatoka wapi.

“Kwa Cityzens, asanteni kwa sapoti yenu isiyo na kikomo. Nawapenda, na nitapambana kila siku kurejea nikiwa na nguvu zaidi, kama shujaa wa Man City.”

Kisha, kwa kauli iliyoibua hofu kwamba ndoto zake za Kombe la Dunia huenda ziko hatarini, aliandika: “Moyo wangu unapiga kwa ajili ya Croatia. Daima! Nitarudi tena, nikiwa bora zaidi kuliko hapo awali. Kwa ajili ya klabu yangu. Kwa ajili ya ndugu zangu wa klabu na timu ya taifa. Kwa ajili ya watu wangu. Kwa ajili ya Croatia.”

Mwenzake Gvardiol, Ruben Dias, naye pia alilazimika kutoka uwanjani kipindi cha pili, huku Guardiola akihisi kuwa ni jeraha la misuli alipoulizwa baada ya mchezo. Man City tayari wamemrejesha beki mwenye umri wa miaka 20, Max Alleyne, kutoka kwenye mkopo wake Watford ili kutoa msaada wa dharura.