Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Petit: Mbappe hakutakiwa Madrid

Muktasari:

  • Mbappe ambaye alitua Madrid baada ya tetesi za muda mrefu zikimhusisha na timu hiyo, amekuwa na wakati mgumu taarifa zikieleza hana maelewano mazuri na baadhi ya wachezaji wenzake.

MADRID, HISPANIA: MCHEZAJI wa zamani wa Ufaransa, Emmanuel Petit anadai Carlo Ancelotti na baadhi ya wachezaji wa Real Madrid hawakutaka kuona Kylian Mbappe anasajiliwa dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu.

Mbappe ambaye alitua Madrid baada ya tetesi za muda mrefu zikimhusisha na timu hiyo, amekuwa na wakati mgumu taarifa zikieleza hana maelewano mazuri na baadhi ya wachezaji wenzake.

Mbali ya kutoelewana na mastaa wenzake, pia Mbappe ambaye tangu kuanza msimu huu amfunga mabao nane katika mechi 16 za michuano yote, amekuwa na shida katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa na ripoti za ndani zinaeleza hana maelewano mazuri na kocha wake, Didier Deschamps.

Mbappe mwenye umri wa miaka 25,  inadaiwa pia hana furaha kwa sababu hachezeshwi eneo analohitaji la upande wa kushoto ambako kwa sasa anacheza Vinicius Jr.

Petit, amefunguka Ancelotti hakuhitaji kufanya maboresho makubwa katika kikosi chake na hakupendekeza kusajiliwa kwa Mbappe lakini huyo aliingizwa katika timu kutokana na utashi wa viongozi.

“Nina uhakika Carlo Ancelotti na wachezaji kadhaa wa Real Madrid hawakutaka timu hiyo imsajili Kylian Mbappe msimu huu. Tayari kilikuwa kikosi ambacho kimeshinda La Liga na Ligi ya Mabingwa na kuingia kwake waliona kungeleta mataitizo. Ancelotti alikuwa  katika nafasi nzuri baada ya kushinda Ligi ya Mabingwa na nadhani angependa wachezaji wawili au watatu kuingia kwenye kikosi chake lakini sio mabadiliko makubwa,” alisema Petit ambaye amewahi kuzicheza, Arsenal, Chelsea, Barcelona na Monaco.

“Tatizo kubwa analokutana nalo Mbappe ni kwamba tayari amekuta wachezaji wawili wakubwa ambao wana malengo kama yake ya kushinda Ballon d’Or nakuwa bora zaidi ambao ni Jude Bellingham na Vinicius Jr.”