Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Peter Lammens amkosha Schmeichel

KIPA Pict

Muktasari:

  • Lammens alijiunga na Man United majira ya kiangazi kwa ada ya Pauni 18 milioni, akichukua nafasi ya Andre Onana, ambaye alitimkia Trabzonspor kwa mkopo dirisha hilo hilo la usajili.

MANCHESTER, ENGLAND: GWIJI wa Manchester United, Peter Schmeichel ametoa maoni yake kuhusu kipa mpya wa klabu hiyo, Senne Lammens alifanya vile ambavyo kipa wa timu kubwa kama hiyo alitakiwa kucheza.

Lammens alijiunga na Man United majira ya kiangazi kwa ada ya Pauni 18 milioni, akichukua nafasi ya Andre Onana, ambaye alitimkia Trabzonspor kwa mkopo dirisha hilo hilo la usajili.

Hata hivyo, Lammens alilazimika kusubiri hadi mwishoni mwa wiki iliyopita kupata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza, baada ya kuwa mchezaji wa akiba nyuma ya Altay Bayindir.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 aliichezea Man United kwa mara ya kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Sunderland kwenye dimba la Old Trafford na alionekana kujiamini licha ya kuokoa mashuti matatu pekee katika mchezo huo.

Uchezaji wake mzuri uliwafanya baadhi ya mashabiki  kumfananisha Schmeichel, jambo lililomuibua gwiji huyo wa kimataifa wa Denmark aliyewahi kuwa kipa wa Man United na alocheza mechi 398 akiwa na kikisi chao,

KI 01
KI 01

"Ukitazama kiwango cha  uchezaji wa magolikipa tuliokuwa nao katika miaka ya hivi karibuni na idadi ya mabao tuliyofungwa kutokana na makosa ya makipa hao ni mengi mno. Nafikiri msimu huu tayari tumepoteza mechi takribani tano kwa makosa ya makipa, wakati nacheza mimi, agizo langu lilikuwa lazima nihakikishe nalinda lango langu na kuisaidia timu kupata walau alama 10 ambazo pengine walitakiwa kuzipoteza ikiwa nisingejizatiti. Hilo ndilo tumekuwa tukikosa kwa miaka michache ya hivi karibuni, makipa wanatoa mabao ya bure na tunapoteza pointi. Kwa hiyo ni vizuri kuona Lammens alichofanya katika mechi yake ya kwanza akiwa anaanza na kutoruhusu bao."

Kauli hiyo ya Schmeichel imekuwa ni tofauti na kile alichokisema hapo awali baada ya kipa huyo kusajiliwa naalikosoa na kusema Man United ilitakiwa isajili kipa mwenye uzoefu kama Emiliano  Martinez au Gianluigi Donnarumma."