Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabosi washtukia jambo Man United, Amorim anahesabu siku

MABOSI Pict

Muktasari:

  • Kumekuwa na sintofahamu katika viunga vya Old Trafford na inaelezwa hata wachezaji wamechoshwa na kocha huyo, huku mwenyewe akikiri siku zake klabuni hapo zinakaribia mwisho na kuwataja wachambuzi kama sehemu ya presha katika timu hiyo.

MANCHESTER, ENGLAND: MABOSI wa Manchester United wameonyesha kuchoka na mwenendo wa kikosi hicho kutokana na matokeo mabaya na sasa wanafikiria hasara watakaoipata ikishindwa kufuzu michuano ya Ulaya msimu ujao na kumfanya Kocha Ruben Amorim kukalia kuti kavu.

Kumekuwa na sintofahamu katika viunga vya Old Trafford na inaelezwa hata wachezaji wamechoshwa na kocha huyo, huku mwenyewe akikiri siku zake klabuni hapo zinakaribia mwisho na kuwataja wachambuzi kama sehemu ya presha katika timu hiyo.

Taarifa kutoka tovuti ya Daily Mail, imefichua mambo yamebadilika na licha ya awali mabosi wa timu hiyo kumuunga mkono kocha huyo kwa asilimia mia, sasa na wao wamechoshwa na matokeo, huku wachezaji wakipoteza imani naye.

Man United imekuwa na matokeo mabovu na wiki iliyopita ilikubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Brentford, kilichowavuruga mabosi hao, wachezaji na hata mashabiki.

Hata hivyo, sababu kubwa iiliyotajwa kumzuia Amorim asifukuzwe ni gharama ya kuvunja mkataba wake kuwa kubwa, ingawa wameona ni bora kuuvunja kuliko kupata hasara endapo timu itashindwa kufuzu michuano ya Ulaya.

AMO 02

Endapo watavunja mkataba wake mwezi huu watalazimika kulipa Pauni 12 milioni kama sehemu ya fidia, ingawa wanaona kiasi hicho ni kidogo ukilinganisha na pesa watakazozikosa ikiwa watafanya vibaya msimu huu na kushindwa kufuzu michuano ya kimataifa mwakani.

Kwa upande wake, akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa kabla ya mechi yao ya Ligi Kuu England dhidi ya Sunderland iliyopigwa jana, Amorim alikiri muda wake katika kikosi hicho unaelekea kumalizika.

"Hakuna mtu  mjinga kati yetu. Tunaelewa tunahitaji matokeo ili kuendelea kuwa hapa. Ikiwa tutaendelea kupata matokeo mabaya, tutafikia hatua ambayo haitowezekana tena kulinda ajira zetu, hii ni klabu kubwa sana na yenye wadhamini wengi pamoja na wamiliki wawili ni ngumu kuendelea kupata matokeo mabaya na kuwa hapa," amesema Amorim na kuongeza,

"Ni ndoto yangu kuwa hapa na nataka kuendelea na kuipigania ili kuendelea. Kinachoniuma zaidi ni kupoteza mechi, siyo kupoteza kazi yangu. Mtu huwa anaogopa kupoteza kazi unapokuwa na bili za kulipa, mimi sina shida hizo, ninapomaliza mechi, siangalii ajira yangu. Kinachoniuma zaidi ni kushindwa kupata ushindi."

AMORIM Pict

Amorim pia amesema moja kati ya changamoto kubwa anazokutana nazo kwa sasa ni maoni ya wachambuzi ambao wamekuwa wakishikilia msimamo wa kwamba mfumo wake una shinda.

Amesema maoni hayo yamekuwa yakiwafikia wachezaji na baadhi wanaamini, jambo linalosababisha yeye na benchi lake la ufundi kuwa na wakati mgumu kila siku kuwaeleza wachezaji shida hasa ilipo ambayo kimsingi sio mfumo.

"Wachezaji wangu wanaamini mnaposema tatizo la timu ni mfumo. Sitaki kubadilisha mawazo yenu, lakini nawaambia tu, wachezaji wangu wanawasikiliza na baadhi huwa wanaweka akilini na kuamini kwani ni kweli tumekuwa hatushindi mechi. Naongea na wachezaji kila siku, nawaeleza hatua kwa hatua tatizo ni nini. Tunapaswa kuangalia sehemu zote za mchezo. Timu hii ilicheza na mifumo tofauti kwa miaka mingi, lakini bado walikuwa wanasema haina utambulisho, kwa hiyo shida siyo mfumo ni mambo madogo madogo tu  ambayo yanaanzia na namna tunavyocheza. Tukibadilisha mfumo kuwa 4-3-3 au 4-4-2 bila kurekebisha vitu fulani, hatutashinda mataji. Huo ndio msimamo wangu."