Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pep Guardiola apewa muda Man City

GUARDIOLA Pict

Muktasari:

  • Guardiola tayari ameshinda mataji 19 akiwa Man City, yakiwemo sita ya Ligi Kuu England na taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya 2023.

MANCHESTER, ENGLAND: MABOSI wa Manchester City wamempa muda wa kufikiria kocha Pep Guardiola kabla ya kujua kama ana mpango wa kumaliza mkataba au kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Kocha huyo kutoka Catalonia, Hispania, ambaye sasa yupo katika msimu wake wa 10 akiwa na Man City, anadaiwa huenda akaondoka mwisho wa msimu huu. Hivi karibuni, Guardiola aliiongoza Man City kutwaa taji la Carabao baada ya kuifunga Arsenal katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Wembley.

Baada ya ushindi huo, taarifa zinaeleza kuwa viongozi wa juu wa klabu hiyo walijaribu kuwasiliana na Guardiola ili kujua kama kocha huyo ana mpango wa kubaki au ataondoka. Man City walitarajia Guardiola kutoa jibu lake, angalau kwa siri, wakati wa mapumziko ya kimataifa ili waweze kujiandaa, lakini hadi sasa kocha huyo bado hajatoa jibu lolote.

Inasemekana kuwa Guardiola ana uhuru wa kuamua mustakabali wake, na klabu tayari ina mpango mbadala iwapo ataondoka mwisho wa msimu.

Vilevile, baadhi ya wachezaji wanaowindwa na Man City, kama Elliot Anderson wa Nottingham Forest, wanataka kujua kama Guardiola ataendelea kuwa kocha kabla ya kufanya maamuzi ya kusaini nao.

Mmoja kati ya makocha wanaotajwa kama mbadala wa Pep ni Enzo Maresca, ambaye awali alifanya kazi kama msaidizi wake kabla ya kuajiriwa na Leicester City, na baadaye Chelsea aliyoipa taji la Kombe la Dunia la Klabu.

Guardiola tayari ameshinda mataji 19 akiwa Man City, yakiwemo sita ya Ligi Kuu England na taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya 2023.