Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Penati yampandisha mzuka Arteta

Muktasari:

  • Tukio hilo ambalo lilitokea dakika ya 59, baada ya Pedro kuubetua mpira juu akiwa ndani ya boksi la Arsenal kisha akapigwa kichwa na William Saliba na kudondoka chini, limeifanya Arsenal kushindwa kufikisha pointi 42 na kuwa na tofauti ya alama tatu dhidi ya vinara Liverpool.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Mikel Arteta amesema penati ya kusawazisha ya Brighton iliyopigwa na Joao Pedro ni uamuzi wa ajabu kuwahi kuushuhudia katika maisha yake yote ya mpira wa miguu na kusisitiza kwamba uamuzi huo uliipunguzia Arsenal nafasi ya kushinda taji la Ligi Kuu England.

Tukio hilo ambalo lilitokea dakika ya 59, baada ya Pedro kuubetua mpira juu akiwa ndani ya boksi la Arsenal kisha akapigwa kichwa na William Saliba na kudondoka chini, limeifanya Arsenal kushindwa kufikisha pointi 42 na kuwa na tofauti ya alama tatu dhidi ya vinara Liverpool.

VAR ndio iliamua kuwa hiyo ilikuwa ni penalti na Pedro akaenda kupiga na kuisawazishia Brighton baada ya kuongoza kwa zaidi ya dakika 60 na Arsenal iliyofunga bao kupitia Ethan Nwaneri kipindi cha kwanza.

Sare hiyo ilikuwa ni ya tatu kwa Arsenal  katika mechi zao sita za ligi zilizopita na sasa inashika nafasi ya pili nyuma ya vinara Liverpool kwa tofauti ya  alama tano, huku Liverpool ikiwa na michezo miwili ya ziada kabla ya jana.

Akizungumza baada ya mechi Arteta alisema: “Ni uamuzi unaosikitisha sana. Sijawahi kuona uamuzi kama huu katika taaluma yangu. Niliwauliza wachezaji kama wamewahi kuona na hakuna aliyewahi kuuona kabla. Unapolitazama tukio hilo, umbali, mchezaji, Joao aligusa mpira na Saliba kwanza aliugusa mpira.” 

Kuhusu suala la usajili usajili, Januari hii, Arteta alisema: “Siwezi kusema tutafanya uamuzi wa kusajili wachezaji baada ya matokeo ya siku moja inabidi tuangalie katika nyanja nyingi.’’

Hata hivyo, kabla ya mchezo huu Arteta alisema anajisikia furaha juu ya kile ambacho wachezaji wake wanakifanya na kusema hana mpango wa kusajili straika.

Katika mchezo huo dhidi ya Palace, Arteta pia alipata pigo zaidi la majeraha baada ya Ethan Nwaneri kutolewa nje kutokana na jeraha la musuli.

Nwaneri alicheza nafasi ya winga wa kulia akiziba pengo la Bukayo Saka ambaye ni majeruhi.