Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Paul Pogba hapa inawezekana

Muktasari:

  • Pogba ambaye awali alifungiwa kucheza soka kwa miaka minne kabla ya hukumu yake kupunguzwa hadi miezi 18 baada ya kukata rufaa, amekuwa katika rada ya timu nyingi duniani ambazo zinahusishwa naye. 

MANCHESTER, MAREKANI: BAADA ya kumaliza kifungo chake cha miezi 18, juzi, sasa ni rasmi kiungo wa zamani wa Manchester United na Juventus yupo huru kusaini mkataba kwa ajili ya kuichezea timu yoyote.

Pogba ambaye awali alifungiwa kucheza soka kwa miaka minne kabla ya hukumu yake kupunguzwa hadi miezi 18 baada ya kukata rufaa, amekuwa katika rada ya timu nyingi duniani ambazo zinahusishwa naye. 

Leo tunakusogezea sehemu tano ambazo kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaweza kutua baada ya kumaliza adhabu.


MANCHESTER UNITED

Pogba aliibua uvumi kuhusu kurejea Man United kwa mara ya tatu baada ya kuweka picha katuni katika ukurasa wake wa Instagram, Januari, mwaka huu, iliyokuwa ikimuonyesha amesimama karibu na Amad Diallo, huku akiwa na jezi ya timu hiyo.

Pogba ambaye aliichezea Man United mechi 233 katika vipindi viwili tofauti, aliondoka Old Trafford 2022 kama mchezaji huru na kurejea Juventus ambako alikwamishwa na majeraha. Hata hivyo, urejeo wake Old Trafford haupewi nafasi kubwa kwa sasa kutokana na mahitaji ya kocha mpya, Ruben Amorim ambaye anaonekana kuwekeza nguvu zaidi kwa mastaa wengine, hasa vijana.


INTER MIAMI

Pamoja na uvumi wa kurejea Man United kumekuwa na tetesi kuhusu nyota huyo kujiunga na Inter Miami inayomilikiwa na David Beckham. Pogba alikutana na Becks kwenye mechi ya ufunguzi ya MLS dhidi ya New York City huko Florida mwezi uliopita jambo lililochochea uvumi kwamba anaweza kujiunga na timu hiyo ya Marekani inayowamiliki mastaa wakubwa kama Lionel Messi, Luis Suarez na Sergio Busquets. Baada ya kukutana na Beckham kupitia Instagram, Pogba aliweka picha kisha akaandika “Tutaona kinachokuja...”


MARSEILLE

Uwezekano wa Pogba kurudi Ufaransa unaonekana kuwa na asilimia kadhaa. Kocha wa Marseille, Roberto De Zerbi alitamka hadharani kwamba angependa kupata huduma ya kiungo huyo kutokana na uwezo wake. “Ningependa kuwa na mabingwa pekee katika timu yangu. Pogba amekuwa bingwa pia, lakini niwe mkweli katika mazungumzo yangu na mabosi hatujawahi kuzungumzia hili.” Mkurugenzi wa Marseille, Mehdi Benatia alikataa kutoa msimamo wake kama anaweza kumsajili Pogba msimu ujao.


SAUDI ARABIA

Nguvu ya kifedha ya Ligi Kuu Saudi Arabia inaweza kumvutia Pogba kufuata nyayo za Cristiano Ronaldo.

Ingawa haionekani ni timu gani anaweza kutua, lakini Pogba anaweza kuvutiwa kuungana na wachezaji wakubwa wa Ufaransa kama N’Golo Kante na Karim Benzema ambao tayari wako Al-Ittihad. Vilevile, Al-Shabab inayosimamiwa na mkurugenzi wa zamani wa Juventus, Pavel Nedved ambaye anamfahamu pia inaweza kuwa chaguo linalowezekana, kwani walishawahi kufanya kazi pamoja. 


FENERBAHCE

Timu hiyo iliripotiwa kuwa inalenga kumsajili Pogba wakati wa dirisha la uhamisho la Januari, mwaka huu, lakini alikuwa katika adhabu. Pogba amewahi kufanya kazi na kocha wa Fenerbahce, Jose Mourinho walipokuwa Man United.

Pogba kama atatua katika timu hiyo atakuwa anaungana na mchezaji mwenzake wa zamani, Mbrazili Fred waliyecheza pamoja Man United.