Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nusu fainali CWC... Tiketi bei chini kuliko glasi ya bia

Muktasari:

  • Bei ya tiketi ya mechi hiyo ilishushwa hadi Dola 13.40, Jumamosi, wakati mwanzoni ilikuwa ikiuzwa Dola 473.90 muda usiozidi siku tatu zilizopita.

MIAMI, MAREKANI: TIKETI kwa ajili ya kipute cha nusu fainali ya Kombe la Dunia la Klabu kati ya Chelsea na Fluminense kitakachopigwa Jumanne zimeshuka na mashabiki wa huko Marekani watakuwa na uwezo wa kuangalia mechi hiyo kwa bei ndogo kuliko glasi ya bia inayouzwa uwanjani.

Bei ya tiketi ya mechi hiyo ilishushwa hadi Dola 13.40, Jumamosi, wakati mwanzoni ilikuwa ikiuzwa Dola 473.90 muda usiozidi siku tatu zilizopita.

Kwa maana hiyo, bei ya tiketi ni rahisi kuliko ya glasi moja ya bia inayouzwa uwanjani MetLife utakapofanyika mchezo huo na bei ya glasi ya bia ni Dola 14.

Ripoti zinafichua uamuzi huo umekuja baada ya Fifa kutaka kuongeza idadi ya mashabiki viwanjani. Fifa imekuwa ikilaumiwa kuanzisha michuano hiyo kwa ajili ya kupata pesa, kitu ambacho kiliwahi kulalamikiwa na aliyekuwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, ambaye alidai ulikuwa mpango wa hovyo ambao unawabana wachezaji.”

Nusu fainali nyingine ya Kombe la Dunia la Klabu itapigwa Jumatano na Paris Saint-Germain itaonyeshana ubabe na Real Madrid katika Uwanja huo wa MetLife, mechi inayotazamiwa kuwa na mvuto mkubwa kutokana na vikosi hivyo vinavyonolewa na makocha Luis Enrique na Xabi Alonso kusheheni mastaa wenye vipaji vikubwa kwenye mchezo wa soka.