Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Paris Saint-Germain yajitosa dili la Ibrahima Konate

Oscar Pict

Muktasari:

  • Konate amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Liverpool kwa muda sasa lakini anadaiwa kutaka kuondoka mwisho wa msimu huu mkataba wake utakapomalizika.

BEKI wa kati wa Liverpool na timu ya taifa ya Ufaransa, Ibrahima Konate, 26, rasmi ameiingiza vitani Paris Saint-Germain ambayo imeonyesha nia ya kutaka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya baridi na kuipiku Real Madrid.

Konate amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Liverpool kwa muda sasa lakini anadaiwa kutaka kuondoka mwisho wa msimu huu mkataba wake utakapomalizika.

Awali, staa huyu alitajwa kuwa na asilimia kubwa za kwenda Madrid, lakini sasa mambo yanaonekana kubadilika baada ya PSG pia kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Konate amekataa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Liverpool licha ya kufanyika kwa majadiliano ya mara kwa mara kati ya wawakilishi wake na mabosi wa Liverpool.

Liverpool inaonekana kuwa tayari kumuuza katika dirisha lijalo badala ya kusubiri kuona akiondoka bure mwisho wa msimu huu.

Tangu kuanza kwa msimu huu Konate amecheza mechi 23 za michuano yote na kufunga bao moja.

Hata hivyo, wakosoaji wamekuwa wakimshambulia Konate kuwa amechangia matokeo ya kusuasua ya Liverpool kwa msimu huu.  


Josh Sargent

WEST Ham United imeongeza jina la mshambuliaji wa timu ya taifa ya Marekani na Norwich City, Josh Sargent, mwenye umri wa miaka 25, katika orodha yao ya wachezaji inaotaka kuwasajili katika dirisha la usajili la Januari.

Sargent amekuwa katika kiwango kizuri huko Championship tangu kuanza kwa msimu huu ambapo amecheza mechi 21 za michuano yote na kufunga mabao saba. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Savinho

MANCHESTER City iko tayari kuwauza wachezaji watatu katika dirisha lijalo la usajili la Januari ili kupata fedha za kufanikisha mipango ya kusajili nyota wapya. Wachezaji wanaotajwa kuwa katika mpango huo ni pamoja na Mbrazili Savinho, 21, beki wa kulia raia wa England, Rico Lewis, 21 na kiungo kutoka Norway, Oscar Bobb, 22. Kuuza wachezaji hao inaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa kocha Pep Guardiola kutaka kujenga upya kikosi chake.


Diogo Dalot

MIAMBA wa Hispania, Real Madrid, wanataka kufanya usajili wa beki wa pembeni wa  Manchester United na timu ya taifa ya Ureno, Diogo Dalot, 26. Dalot anatajwa kulivutia benchi la ufundi la Madrid kutokana na uwezo wake wa kucheza pande zote kuanzia beki wa kulia na kushoto jambo ambalo litasaidia timu hususani kutakapota na majeraha. Mkataba wake unamalizika mwaka 2028.


Yann Sommer

INTER Milan imeanza kuangalia majina ya makipa watakaoweza kuchukua nafasi ya kipa wao raia wa Uswisi, Yann Sommer, 36, anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Miongoni mwa makipa wanaotajwa sana ni Guglielmo Vicario, 29,   wa Tottenham na timu ya taifa ya Italia. Hata hivyo, ili kumpata Inter  itatakiwa kuweka kiasi kikubwa cha pesa mezani kwani bado ana mkataba wa hadi 2028.


Pedro Porro

TOTTENHAM Hotspur iharakisha mazungumzo ya mkataba mpya na wawakilishi wa beki wa kulia kutoka Hispania, Pedro Porro, 26, baada ya kuona Manchester City inatamani kumsajili.

Porro amekuwa mhimili muhimu katika mfumo wa Spurs, sasa Man City ilitamani kumsajili tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini ilishindikana. Mkataba wake wa sasa unaisha 2028.


Raheem Sterling

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Raheem Sterling, 31, anaweza kupewa ruhusa ya kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya baridi ikiwa ni sehemu ya timu hiyo kufanya mabadiliko. Hadi sasa Leeds United na Crystal Palace zinatajwa kuonyesha nia ya kumsajili nyota huyo mwenye uzoefu mkubwa wa Ligi Kuu, ambaye kwa sasa hapati nafasi ya kucheza kwa matajiri hao wa London.ataba wa fundi huyu unamalizika mwaka 2027.


Joshua Zirkzee

AC Milan imeelekeza macho yake kwa mshambuliaji wa West Ham na timu ya taifa ya Ujerumani, Niclas Fullkrug 32, baada ya kuona mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Man United na timu ya taifa ya Uholanzi, Joshua Zirkzee, 24, una asilimia chache za kufanikiwa. Milan inaona kumpata Zirkzee ni ngumu sana kutokana na aina ya mfumo wa malipo.

Mkataba wa Fullkrug  unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.