Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Palmer atetewa kukosa penalti

Muktasari:

  • Palmer, 22, hajafunga bao lolote katika mechi tisa kabla ya kipute hicho cha Jumapili dhiid ya Leicester City, ambayo iliwasili Stamford Bridge ikiwa na kazi moja ya kutafuta pointi za kuwafanya kubaki kwenye Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca amemtetea staa wake Cole Palmer kwa kukosa penalti dhidi ya Leicester City akidai kwamba kiungo huyo mshambuliaji aliumwa kabla ya mechi.

Palmer, 22, hajafunga bao lolote katika mechi tisa kabla ya kipute hicho cha Jumapili dhiid ya Leicester City, ambayo iliwasili Stamford Bridge ikiwa na kazi moja ya kutafuta pointi za kuwafanya kubaki kwenye Ligi Kuu England.

Palmer alipata nafasi ya kumaliza ukame wake wa mabao baada ya Chelsea kupata penalti kwenye kipindi cha kwanza na yeye kwenda kupiga, lakini kipa wa Leicester City, Mads Hermansen, alimgomea.

Marc Cucurella alimwokoa Palmer kwa kufunga bao pekee katika mechi hiyo na kuipa ushindi Chelsea, ambao uliwasaidia kupanda hadi nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu England, wakiiengua Manchester City kwenye mbio za kufukuzia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Palmer kushindwa kufunga mkwaju wa penalti tangu alipoanza kucheza soka la timu ya wakubwa. Lakini, kocha Maresca alisema baada ya mechi hiyo kwamba mkali huyo wa zamani wa Man city alikosa mazoezi kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya tumbo, hivyo alicheza mechi hiyo akiwa hayupo fiti kwa asilimia 100.

Alisema: "Cole hakufanya mazoezi. Hakuwa akijisikia vizuri. Aliamka na kuniambia anataka kucheza kusaidia timu ili ipate tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

"Kwa siku mbili, alikuwa akisumbuliwa na homa, mnasemaje kwa Kiingereza - kuharisha. Alikuwa vibaya sana. Lakini, alitaka kucheza kuonyesha kile anachoweza kukifanya. Alijitolea kila kitu. Kuhusu penalti atakwenda kukosa nyingi sana kwenye maisha yake. Anatupa furaha. Watu wanapaswa tu kufahamu jinsi anavyojitolea. Cole ni mchezaji wa kiwango cha juu."