Osimhen afungia vioo timu za EPL

LONDON, ENGLAND . NYOTA wa Napoli, Victor Osimhen, amesisitiza anafurahia maisha kwenye klabu hiyo licha ya kuhusishwa na timu za Ligi Kuu England, Manchester United ikitajwa.
Fowadi huyo wa kimataifa wa Nigeria amekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu, kutokana na mchango wake Napoli kuelekea katika mbio za ubingwa wa Serie A, na amefunga mabao 21 katika emechi 24 za ligi.
Kwasasa Napoli ipo kileleni kwenye msimamo wa Serie A kwa uwiano wa pointi 14 dhidi ya wapinzani wao Lazio ambao wana pointi 61 huku wakijiweka katika nafasi nzuri ya kubeba ubingwa.
Kiwango cha Osimhen cha upachikaji wa mabao ndio kiwamewavutia timu nyingi za Ulaya, Man United ikitajwa kuwa na nia ya kumsajili dirisha la usajili la kingazi.
Aidha, Osimhen akaweka wazi kwamba ana furaha kukipiga katika klabu yake sasa kwani mashabiki wanamkubalika tangu alipojiunga mwaka 2020.
"Tuko karibu na malengo yetu, tulisubiri kwa muda mrefu," Osimhen aliiambia tovuti ya TG5 wakati akizungumzia mipango ya Napoli kuelekea katika ubingwa wa Serie A.
"Wachezaji waliamini kila wakati, tulifikiri kila wakati tunaweza kufanya kitu cha kipekee, hata wakati hakuna mtu mwingine aliyeamini tunaweza. Upendo wao kwangu ni wa ajabu, sijawahi kupokea upendo kama huu, nachotaka ni kusherehekea mafanikio yetu uwanjani pamoja." alisema Osimhen Mwezi uliopita Osimhen alifichua siri kwamba ana ndoto ya kucheza katika moja ya timu kubwa kutoka Ligi Kuu England, huku mashabiki wakiwa na shauku ya kufahamu huenda staa huyo akatimkia England.
Osimhen alirejea kwenye mechi ya Napoli waliyosuluhu dhidi ya Hellas Verona baada ya kupona majeraha, aidha baada ya mtanange huo wa Serie A timu hiyo inajiandaa kucheza mechi ya pili ya marudiano ya robo fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan, mechi ya kwanza Napoli ilifungwa bao 1-0.