Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

He! Enzo Fernandez atafuta nyumba Madrid

ENZO Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo bado ana mkataba wa miaka saba huko Stamford Bridge, lakini kwa siku za karibuni amekuwa akihusishwa na Klabu ya Real Madrid na huenda akanaswa dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

MADRID, HISPANIA: STAA wa Chelsea, Enzo Fernandez ameripotiwa kuanza kutafuta nyumba huko Hispania, jambo linaloibua utata kwamba huenda Muargentina huyo ana mpango wa kuondoka Stamford Bridge.

Kiungo huyo bado ana mkataba wa miaka saba huko Stamford Bridge, lakini kwa siku za karibuni amekuwa akihusishwa na Klabu ya Real Madrid na huenda akanaswa dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Kocha mtarajiwa wa Real Madrid, Xabi Alonso ambaye atakwenda kuchukua mikoba ya Carlo Ancelotti huko Bernabeu, anataka kutengeneza timu itakayokuwa na kiungo bora kabisa.

Na mwandishi Gustavo Mendez aliripoti kwamba Fernandez na mpenzi wake walionekana wakitafuta nyumba wiki hii huko Hispania.

Mendez alidai kwamba Fernandez na mabingwa hao mara 15 wa Ulaya wamefikia makubaliano, lakini bado hayajathibitisha.

Staa huyo wa Ligi Kuu England aliripotiwa kuelekezwa eneo la kwenda kutafuta nyumba na Muargentina mwenzake, Julian Alvarez, ambaye anakipiga kwenye kikosi cha Atletico Madrid.

Fernandez, 24, alikuwa kwenye rada za Real Madrid kabla ya kujiunga na Chelsea, kwa ada iliyoweka rekodi ya uhamisho Uingereza kwa wakati huo, Pauni 106 milioni aliponaswa kutoka Benfica mwaka 2023.

Miamba hiyo ya La Liga ilionyesha pia dhamira ya kumsajili mkali huyo kwenye dirisha la Januari, lakini kocha wa Chelsea, Enzo Maresca anamtaka abaki Stamford Bridge. Lakini, kinachoelezwa ni kwamba kama Fernandez atashindwa kupatikana, basi Madrid itahamia kwa viungo Alexis Mac Allister wa Liverpool na Hudo Larsson wa Eintracht Frankfurt.