Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luka Modric anatajwatajwa Swansea City

LUCA Pict

Muktasari:

  • Katika taarifa hiyo iliyojaa hisia nyingi kiungo huyo mwenye umri wa miaka 39 alithibitisha kwa kubainisha kwamba umefika wakati wa kuachana na miamba hiyo ya Hispania.

MADRID, HISPANIA: KIUNGO Luka Modric na klabu ya Real Madrid wametangaza kwamba staa huyo ataachana na maisha ya Bernabeu baada ya kukamilika kwa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu.

Katika taarifa hiyo iliyojaa hisia nyingi kiungo huyo mwenye umri wa miaka 39 alithibitisha kwa kubainisha kwamba umefika wakati wa kuachana na miamba hiyo ya Hispania.

Modric amekuwa kwenye klabu ya Real Madrid tangu 2012 na amefanikiwa kunasa mataji 28, ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya mara sita, La Liga mara nne, Copa del Rey mara mbili na Klabu Bingwa Dunia mara sita.

Lakini, staa huyo wa zamani wa Tottenham ameelezwa kwamba anaweza kushtua wengi kwa kuhama kutoka kwenye timu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hadi kwenye Championship kwa kwenda kujiunga na Swansea, timu ambayo Modric anaripotiwa kuwa ni mmiliki mwenza.

Straika wa zamani wa Real Madrid, Fernando Morientes ameunga mkopo mpango wa Modric kwenda kujiunga na klabu hiyo ya Wales msimu ujao.

Morientes alisema: “Luka Modric kuichezea Swansea itakuwa safi sana. Nina hakika kitakwenda kuwa kitu chenye kufurahisha kwa mashabiki. Mchezaji kama Luka Modric, hata kama yupo kwenye zama za mwisho za maisha yake, kwenda kuchezea timu yao.”