Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Oscar afikiria kutundika daruga

Oscar Pict

Muktasari:

  • Staa huyo wa zamani wa Chelsea alifanyiwa uchunguzi wa kina wa afya yake baada ya kuanguka mazoezini mwezi uliopita.

RIO DE JANEIRO, BRAZIL: MSHINDI mara mbili wa taji la Ligi Kuu England, kiungo wa Kibrazili Oscar ameripotiwa kuwa na mpango wa kustaafu soka kutokana na kuwa na tatizo kubwa ya kiafya.

Staa huyo wa zamani wa Chelsea alifanyiwa uchunguzi wa kina wa afya yake baada ya kuanguka mazoezini mwezi uliopita.

Aliwahishwa hospitali baada ya kupoteza fahamu wakati alipokuwa akifanya mazoezi ya kuendesha mashine inayofanana na baiskeli. Oscar kwa sasa ni mchezo wa Sao Paulo, klabu ambayo ndiyo aliyoibukia utotoni.

Mkali huyo mwenye umri wa miaka 34 hajafanya mazoezi tangu alipopatwa na tukio hilo na sasa anafikiria kustaafu.

Kwa mujibu wa Globo, Oscar ameanza kuzungumzia hatima yake kwenye klabu hiyo na anafikiria kustaafu na hilo anaweza kulitangaza rasmi siku chache zijazo. Na kama ataamua kustaafu, basi ataondoka kwenye soka akiwa mwenye hadhi kubwa, hasa kwa kipindi chake alichokuwa huko Chelsea.

The Blues ilimsainisha Oscar kutoka Internacional mwaka 2012 na alicheza Stamford Bridge kwa kipindi cha misimu minne na nusu. Alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Chelsea chini ya Jose Mourinho kilichobeba ubingwa 2014/15, alipokuwa akicheza Namba 10 nyuma ya straika Diego Costa.

Licha ya kwamba aliondoka katikati ya msimu 2016/17 na Chelsea ilichukua ubingwa chini ya kocha Antonio Conte, Oscar alikabidhiwa medali ya ubingwa kutokana na kucheza mechi nane kati ya Agosti na Januari na ilizidi idadi ya mechi tano zinazotakiwa kwa mchezaji ili kupata medali ya ubingwa.

Zaidi ya hilo, alishinda Europa League na Kombe la Ligi wakati akiichezea Chelsea. Kisha Oscar alienda China kuitumikia Shanghai Port kwa miaka saba, kabla ya kurudi Sao Paulo, Krismasi mwaka jana na kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Kwenye soka la kimataifa, Oscar ameitumikia Brazil mara 48 kati ya 2011 na 2015.