Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kali ya Neymar Brazil amgeukia “Dr Miracle

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa zamani wa Barcelona na Paris Saint-Germain, Neymar 33, amekuwa akipambana na tatizo la maumivu ya goti tangu alipojiunga na klabu ya utotoni mwake Santos akitokea Al-Hilal kwenye dirisha la Januari mwaka huu.

RIO DE JANEIRO, BRAZIL: SUPASTAA, Neymar amemgeukia “Dr Miracle” kuamua hatima yake ili kutimiza ndoto za kucheza Kombe la Dunia 2026.

Fowadi huyo wa zamani wa Barcelona na Paris Saint-Germain, Neymar 33, amekuwa akipambana na tatizo la maumivu ya goti tangu alipojiunga na klabu ya utotoni mwake Santos akitokea Al-Hilal kwenye dirisha la Januari mwaka huu.

Neymar aliumia goti wakati alipokuwa uwanjani kuitumikia Brazil, Oktoba 2023. Na sasa anajiandaa kufanyiwa upasuaji mkubwa baada ya kukiuka ushauri wa daktari wakati alipoamua kucheza na maumivu ili kuisaidia Santos isishuke daraja msimu huu. Neymar alivaa buti zake akifunga mabao matano na asisti moja katika mechi nne za mwisho, hivyo kuisaidia Santos kukwepa kasheshe la kushuka daraja.

Kiwango chake bora kimewafanya mashabiki sasa kumtaka kocha wa Brazil, Carlo Ancelotti kumjumuisha Neymar kwenye kikosi chake kitakachokwenda kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia 2026 zitkazofanyika Marekani, Mexico na Canada.

Na Neymar sasa anataka kuzifanya ndoto zake kutimia kwa kumgeukia daktari ambaye amekuwa akifanya maajabu mengi kwenye kuwatibu wanasoka kwa kutimia njia zake zisizoelezeka.

Fiziotherapisti wa Kibrazili, Dr Eduardo Santos anatazamwa kama mkufunzi wa tiba ya kisayansi kwa wanamichezo amekuwa akifanya kazi na klabu za Shanghai SIPG, Zenit St Petersburg na Vitesse Arnhem.

Kwa sasa maskani yake ipo England, ambako anamsaidia straika wa Fulham, Rodrigo Muniz kurejea uwanjani kwa haraka kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli aliyopata mwezi uliopita. Na siku za hivi karibuni, Santos alifanya kazi na staa wa Manchester United, Matheus Cunha na beki wa Monaco, Vanderson.

Wachezaji wengine aliowahi kuwatibu huko nyuma ni Philippe Coutinho, Oscar na Hulk. Neymar sasa anaamini Santos, ambaye amepachikwa jina la “Dr Miracle” anaweza kufanya miujiza yake na kumfanya apone kwa haraka kama ambavyo aliwahi kufanya kwa beki wa zamani wa Chelsea na Arsenal, David Luiz.

Beki wa Kibrazili, Luiz, ambaye kwa kipindi hicho alikuwa PSG aliumia goti na alitakiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda usiopungiua wiki 10 mwaka 2015, lakini Santos alimsaidia na kurudi uwanjani ndani ya siku 10 tu.

Neymar sasa anaamini goti lake litapata ufumbuzi wa kitiba kwa haraka ili kumfanya fiti kabla ya kuanza kwa msimu mpya kwenye soka la Brazil mwishoni mwa Januari. Mpango wake ni kurejea kwenye kikosi cha Brazil, ambacho mara ya mwisho alikitumikia mwaka 2023. Lakini, kocha Ancelotti alisema hawezi kutoa upendeleo wowote katika suala la kuteua kikosi chake kitakachokwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.

Kocha huyo Mtaliano alisema: “Kuna wachezaji wengi sana ambao ni wazuri, hivyo nahitaji mchezaji ambaye atakuwa fiti kwa asilimia 100%. Sio Neymar tu, hii inaweza kuwa hata kwa fowadi wa Real Madrid, Vinicius.

“Kama Vinicius atakuwa fiti kwa asilimia 90%, nitamwita mchezaji mwingine ambaye atakuwa fiti kwa asilimia 100%, kwa sababu hii timu ushindani upo kwenye kiwango cha juu sana, hasa pale mbele. Mbele kuna wachezaji wengi wazuri.”

Aliongeza: “Kama tunamzungumzia Neymar, itatubidi tuzungumzie wachezaji wengine pia. Lazima tuifikirie Brazil, ambayo inaweza kuwa na Neymar au bila Neymar, iwe na wachezaji wengine au isiwe na wachezaji wengine. Kikosi chetu kitafanyika baada ya mechi za Fifa Machi. Kama Neymar atastahili, kama atakuwa fiti kuliko mtu mwingine, atakwenda kucheza Kombe la Dunia. Sitaki kumwahidi mtu yeyote.”