Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri ya mke wa Fabinho na Anfield

SHOWBIZ Pict
SHOWBIZ Pict

Muktasari:

  • Rebeca ni mwanamke anayejipenda na kuiweka mbele familia yake lakini mapenzi yake katika soka bado yako pale pale, mashabiki wa Liverpool na viunga vyake vya Anfield wanaweza kusimulia kwa ufasaha zaidi.

NI siku chache zimepita tangu kiungo wa zamani wa Liverpool, Fábio Henrique Tavares maarufu kama Fabinho, 32, kumtakia heri ya kuzaliwa mkewe Rebeca Tavares, 30, mwanasoka aliyestaafu mapema ili kuwa karibu na mumewe.

Rebeca ni mwanamke anayejipenda na kuiweka mbele familia yake lakini mapenzi yake katika soka bado yako pale pale, mashabiki wa Liverpool na viunga vyake vya Anfield wanaweza kusimulia kwa ufasaha zaidi.

"Heri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu (Rebeca)!. Mungu akubariki na atimize ndoto zako katika maisha yako. Asante kwa kuwa ngome yetu ya usalama," alieleza Fabinho na kuongeza.

"Ni jambo la kipekee sana kukupata kama mke na mama wa watoto wetu. Nakupenda mpenzi wangu!" alisema Fabinho, mzaliwa wa Campinas, Brazil. 

SHOW 01

Fabinho ambaye mara nyingi huitwa Flaco, jina linalomaanisha (mtu) mwembamba kwa Kihispania, alifunga ndoa na Rebeca mwaka 2015, baada ya kuwa pamoja katika uhusiano tangu 2013.

Hata hivyo, vyanzo vingi vya habari na machapisho mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, vimetaja tu mwaka wa wao kufunga ndoa lakini tarehe kamili, yaani siku na mwezi haijawekwa wazi.

Mnamo Julai 2022, ndipo walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza ambaye alikuja kuzaliwa Desemba 31, 2022 na kupewa jina la Israel, huku wa pili, Alicia akizaliwa Agosti 4, 2024.

SHOW 02

Rebeca alimpa binti yake jina hilo kutokana yeye ni shabiki mkubwa wa Alicia Keys, mwanamuziki kutokea Marekani aliyetamba na nyimbo kama No One (2007), Girl on Fire (2012) na  You Don't Know My Name (2003).

Mara zote taarifa za kuzaliwa kwa watoto wao wamekuwa wakizitoa kupitia mitandao ya kijamii ambapo wana wafuasi wengi wanaovutiwa zaidi na mtindo wao wa maisha kama familia yenye umoja na upendo.

Awali, Rebeca alikuwa mwanasoka na alicheza kama mshambuliaji nchini Hispania, kisha akasaini mkataba na AS Monaco FF ya Ufaransa mnamo Januari 2018 kabla ya kustaafu mwaka huo huo ili kumuunga mkono mumewe.

Kwa kipindi chote amekuwa bega kwa bega na Fabinho - wakihama wote kuanzia Ufaransa, Uingereza hadi sasa Saudi Arabia ambapo mchezaji huyo anakipiga katika klabu ya Al-Ittihad inayoshiriki Saudi Pro League.

SHOW 03

Wakati Fabinho anajiunga na Liverpool mnamo Mei 2018 kwa dau la Pauni39.3 milioni, Rebeca alifurahi sana kuona mume wake anaenda kucheza Ligi Kuu England (EPL) kwa mara ya kwanza tena katika klabu kubwa.

Rebeca aliposti video kwenye Insta Stories akionyesha safari yao wakielekea Liverpool kukamilisha usajili wa mume wake, kisha akaandika "Let’s go Reds", msemo wa hamasa unaotumiwa na klabu hiyo.

"Tuko kwenye kutua za mwisho kutua Liverpool, bado dakika chache, unajisikiaje?" Rebeca alimuuliza mumewe. Naye Fabinho akajibu, "najihisi vizuri sana,".

SHOW 04

Na baada ya kutangazwa rasmi kwa usajili wake, Fabinho, Rebeca na watu wao wengine waliokuwa nao pamoja kwenye ndege walisherehekea mafanikio hayo.

"Hongera baby, sasa sisi ni Reds," alisema Rebeca, kabla ya kupiga picha akiwa amevaa jezi ya Liverpool huku akibusu nembo ya klabu hiyo iliyotwaa EPL mara 20, na Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CL) mara tatu.

Hata hivyo, ni kama usajili ya Fabinho ulikuwa wa kimya kimya, kwani aliwasili Liverpool ndani ya saa 48 baada ya timu hiyo kupoteza fainali ya UEFA CL dhidi ya Real Madrid, ila baadaye mambo yalienda vizuri. 

Fabinho akiwa na Liverpool alishinda mataji mengi - EPL 2019/20, UEFA CL 2018/19, FA Cup 2021/22, EFL 2020/21, Ngao ya Jamii 2022, UEFA Super Cup 2019, na FIFA Club World Cup 2019.

SHOW 05

Msimu wa 2021/22, huenda ndio uliokuwa bora zaidi kwake - akifunga mabao manane kama kiungo mkabaji na kusaidia Liverpool kushinda mataji mawili.

Baada ya miaka yake mitano akiwa Anfield, Fabinho alihamia Al-Ittihad kwa ada ya Pauni40 milioni. Na huko nako amefanya vizuri akishinda taji la Saudi Pro League 2024/25, na Kombe la Mfalme 2024/25.

Hata hivyo, Rebeca hakuwa tayari kwa uhamisho huo wa kwenda Al-Ittihad!. Alitumia Instagram akieleza kuwa mapenzi yake bado yako kwa Liverpool.

"Nahisi mapigo ya moyo wangu yanaenda kasi sana... Sikuwa tayari kuaga (na bado siko tayari) lakini haya ndio maisha, ndivyo soka lilivyo," alieleza Rebeca na kuongeza.

"Tumeandika historia nzuri hapa. Historia ambayo pia imeandikwa katika mnara. Reds daima, Reds tutaonana tena. Mwanangu atakujua, Anfield, na asanteni wote kwa sapoti na upendo wenu," alisema.

Kutokana na kile ambacho Fabinho na Rebeca waliandika katika mitandao ya kijamii wakati wakiaga, ni wazi kwamba Liverpool itabaki kuwa na sehemu maalum katika nyoyo zao kwa miaka yote.

Sasa akiendelea na maisha huko Saudi Arabia, katika toleo lijalo tutamuangazia kiundani Rebeca katika soka la wanawake ambapo anamtaja 'lejendi' wa Brazil na Barcelona, Ronaldinho kama 'role model' wake.