Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Onana aharibu hesabu mapema

ONANA Pict

Muktasari:

  • Onana, 29, alipata maumivu hayo wakati aliporejea mazoezini Man United wiki iliyomalizika huko Carrington. Uchunguzi wa awali wa majeraha hayo yaliyompata Onana yanaripotiwa yanaweza kumweka nje ya uwanja kwa wiki hadi nane - jambo litakalomfanya akosekane kwenye ziara ya mechi za kujiandaa na msimu mpya zitakazofanyika Marekani.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imepata pigo kubwa baada ya kipa Andre Onana kupata maumivu ya misuli ya paja itakayomfanya akosekane kwenye ziara ya pre-season ya miamba hiyo.

Onana, 29, alipata maumivu hayo wakati aliporejea mazoezini Man United wiki iliyomalizika huko Carrington. Uchunguzi wa awali wa majeraha hayo yaliyompata Onana yanaripotiwa yanaweza kumweka nje ya uwanja kwa wiki hadi nane - jambo litakalomfanya akosekane kwenye ziara ya mechi za kujiandaa na msimu mpya zitakazofanyika Marekani.

Majeraha hayo ya Onana yana maana staa huyo atakuwa na mlima mrefu wa kupanda katika kujiweka fiti kabla ya mechi ya kwanza ya msimu kwenye Ligi Kuu England na Man United itakipiga na Arsenal, Agosti 17.

Hilo linampa maumivu ya kichwa Kocha Ruben Amorim na sasa timu hiyo kwenye usajili wake wa dirisha hili italazimika kuweka ubaoni pia mpango wa kusajili kipya mpya.

Onana amekuwa kwenye mijadala mingi kuhusu hatima yake kwenye kikosi cha Man United kutokana na makosa mengi anayofanya golini tangu aliponaswa kwa ada ya Pauni 47 milioni akitokea Inter Milan. Kwamba ripoti zinafichua Man United ipo tayari kumuuza kwa Pauni 30 milioni.

Onana aliwekwa kando na kocha Amorim baada ya makosa aliyofanya kwenye Europa League dhidi ya Lyon, lakini baadaye alimrudisha kwenye kikosi na kuendelea kuwa kipa namba moja.

Kwa kipindi hiki cha dirisha la usajili, Man United imekuwa ikihusishwa na kipa wa Asto Villa, Emiliano Martinez, ambaye anaonekana kutaka kuachana na maisha ya Villa Park.

Man United itacheza mechi yao ya kwanza ya pre-season, Jumamosi ijayo dhidi ya Leeds United huko Stockholm baada ya hapo itakwenda Marekani, ambako itamenyana na West Ham, Bournemouth na Everton.