Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Olmo, Pau kizungumkuti FC Barcelona

OLMO Pict

Muktasari:

  • LaLiga ilikubali uandikishaji wa wachezaji hao wawili Januari mwaka huu baada ya Barca kutangaza kuuza tiketi za viti 475 vya VIP kwa wawekezaji kadhaa kutoka Mashariki ya Kati kwenye uwanja mpya wa Camp Nou ambao unatarajiwa kufunguliwa kabla ya kumalizika kwa msimu huu.

BARCELONA, HISPANIA: NYOTA wa Barcelona, Dani Olmo na Pau Victor wanakabiliwa na hatari ya kuondolewa tena kikosini na mamlaka za soka nchini Hispania baada ya kunusurika kadhia hiyo mwaka jana.

LaLiga ilikubali uandikishaji wa wachezaji hao wawili Januari mwaka huu baada ya Barca kutangaza kuuza tiketi za viti 475 vya VIP kwa wawekezaji kadhaa kutoka Mashariki ya Kati kwenye uwanja mpya wa Camp Nou ambao unatarajiwa kufunguliwa kabla ya kumalizika kwa msimu huu.

Barca ilieleza kwamba matajiri hao wamenunua viti kwa muda wa miaka 30 ambapo wametoa Pauni 84 milioni kiasi ambacho ndio kilitumika kutimiza hesabu za kifedha za La Liga na baadaye wakaruhusiwa kuwachezesha Pau na Olmo ingawa ushahidi huo ulipitishwa na mahakama kwani La Liga ilishakataa.

Hata hivyo, imebainika kwamba nyaraka zinazothibitisha makubaliano hayo zilifanywa na mhasibu wa zamani aliyetumwa na klabu Desemba, 31, baada ya makubaliano yake na kampuni ya kimataifa ya Grant Thornton kumalizika.

Lakini, wakati kampuni mpya ya uhasibu ya Barcelona, Crowe Spain, ilipowasilisha takwimu rasmi za msimu huu kufikia tarehe ya mwisho ya mwezi uliopita, hakuna hata kiasi kimoja cha fedha kilichojumuishwa kwamba kiliingizwa kama mapato jambo ambalo La Liga wanaona kuna udanganyifu ulifanyika juu ya ununuzi wa viti hivyo 475.

Katika taarifa yao LaLiga ilitangaza: "Mnamo Januari 3, 2025, cheti kilichotolewa na mdhibiti mpya wa klabu kikithibitisha kuwa muamala huo ulirekodiwa ipasavyo kama mapato kwenye akaunti ya Faida na Hasara ya klabu kwa msimu huu. Dokumenti hii ilikuwa muhimu na ya msingi ili kuthibitisha uhalali wa wachezaji husika kucheza lakini baadaye katika taarifa ya nusu msimu iliyotolewa na mhasibu mpya ilionyesha kwamba kiasi hicho cha pesa hakikuwepo na hakikurekodiwa katika akaunti ya hasara na faida za timu. Hii inakwenda kinyume cha kile kilichothibitishwa na Klabu na mdhibiti hapo awali."

Matokeo yake ni kwamba LaLiga iliijulisha Barcelona kwamba upungufu katika hesabu zao bado upo palepale na mkaguzi wa hesabu aliyefanya hesabu hizo ameripotiwa katika mamlaka husika kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Barca ipo katika vita ya kuwania ubingwa msimu huu ambapo inashika nafasi ya kwanza mbele ya Real Madrid inayoshika nafasi ya pili nyuma ya Barca kwa tofauti ya pointi tatu.

Madrid pia huenda ikafungua kesi kutaka haki juu ya wachezaji ambao walicheza mechi nyingi za Barca wakati hawakuwa na uhalali wa kufanya hivyo kama La Liga ilivyothibitisha.

Olmo ameshacheza mechi saba za LaLiga ambazo sita zilimalizika kwa Barca kushinda na moja ikaisha kwa sare pia amecheza mechi tatu za Copa del Rey, mechi ya Super Cup ya Hispania na mbili katika Ligi ya Mabingwa tangu Januari. Victor ameonekana kwenye mechi tano jumla mwaka huu.