Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Olmo bado kizungumkuti, sita zinamtaka

Olmo Pict

Muktasari:

  • Barcelona ilitoa Pauni 50 milioni kwenda RB Leipzig kwa ajili ya kumsajili Olmo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

BARCELONA, HISPANIA: RIPOTI zinaeleza, timu sita za Ligi Kuu, England ziko tayari kupambana kumsajili kiungo wa Barcelona, Dani Olmo kwa usajili huru katika dirisha hili.

Barcelona ilitoa Pauni 50 milioni kwenda RB Leipzig kwa ajili ya kumsajili Olmo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Lakini hali yao mbaya ya kiuchumi ilisababisha asajiliwe kwa kibali maalumu katika mfumo usajili ya chjama cha soka kwa nusu ya kwanza ya msimu kwa sababu kanuni zilikuwa haziwaruhusu.

Barca ipo katika vizuizi vikali vilivyowekwa na La Liga kupitia kanuni zao ambazo zinaitaka timu kutumia sawa na ilichokiingiza, hivyo Barca inayokabiliwa na deni la Pauni 1 bilioni, ili kuweza kumtumia OImo kwa nusu ya msimu iliyosalia.

Baada ya kumsajili mwaka jana, La Liga ilitoa ruhusa maalum kumjumuisha Olmo, mwenye umri wa miaka 26, kwenye kikosi chao hadi Desemba 31 na baada ya hapo iliitaka Barca kutuma maombi ya kumjumuisha tena lakini wakiwa na vielelezo vinavyoonyesha kwamba uchumi wao umeinuka.

Hata hivyo, Barcelona imewasilisha maombi mara mbili lakini yote yalikataliwa, hivyo staa huyu anaweza kuondoka bure kama mwafaka hautopatikana juu ya yeye kucheza kwa nusu msimu iliyobakia kwa sababu katika mkataba wake kuna kipengele kinachomruhusu kuondoka bure ikiwa hataweza kucheza na ripoti zinasema jina lake limeshaindolewa kwenye mfumo wa La Liga. 

Kwa mujibu wa ripoti za Hispania, hadi kufikia sasa timu zote sita zinataka kumsajili mara tu suala la kucheza litakaposhindikana.

Liverpool, Chelsea na Tottenham wanatajwa kuwa tayari wanamfuatilia mchezaji huyo pamoja na  Manchester United, Man City, na Arsenal.