Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ola Aina afichua sababu za kuikacha England na kuichagua Nigeria

AINA Pict

Muktasari:

  • Aina (29), ambaye alizaliwa jijini London na wazazi wenye asili ya Nigeria, alionekana kuwa na mustakabali mzuri na timu ya taifa ya England maarufu Three Lions baada ya kupita katika ngazi mbalimbali za vijana kuanzia U16 hadi U20.

BEKI wa pembeni wa Nottingham Forest, Ola Aina, ameweka wazi sababu zilizomfanya kuchukua uamuzi wa kubadili uraia wake na kuanza kuichezea timu ya taifa ya Nigeria badala ya England.

Aina (29), ambaye alizaliwa jijini London na wazazi wenye asili ya Nigeria, alionekana kuwa na mustakabali mzuri na timu ya taifa ya England maarufu Three Lions baada ya kupita katika ngazi mbalimbali za vijana kuanzia U16 hadi U20.

Licha ya kucheza zaidi ya michezo 20 akiwa na timu za vijana za England na kuitwa kikosi cha U21 mwaka 2015, nyota huyo wa zamani wa Chelsea hakuwahi kuichezea timu ya wakubwa ya England.

AIN 01

Mnamo Machi 2017, alikubali mwaliko wa kufanya mazoezi na kikosi cha Nigeria jijini London, jambo ambalo lilikuwa mwanzo wa safari yake mpya.

Baada ya kupata baraka za FIFA kubadili uraia wake, Aina alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na Super Eagles mnamo Oktoba 2017 dhidi ya Zambia katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.

Akizungumza kupitia chaneli ya YouTube ya klabu ya Nottingham Forest, Aina ameeleza kuwa asili yake na shinikizo la kifamilia vilichukua nafasi kubwa katika uamuzi huo.

"Nilizaliwa na kukulia London, lakini nilichagua kuichezea Nigeria. Ulikuwa ni uamuzi nilioufanya nikiwa na umri wa miaka 20. Huko ndiko wazazi wangu walikotoka, huo ndio urithi wangu," amesema Aina.

AIN 02

Ameongeza kuwa fursa hiyo ilipojitokeza, alihisi ni wakati sahihi wa kuipokea kwa moyo mmoja.

Beki huyo ameeleza kuwa, kuvaa jezi ya kijani na nyeupe ya Nigeria huleta furaha isiyo na kifani kwa familia yake.

"Familia yangu inajivunia sana mimi, hususan ninapovaa jezi ya Super Eagles. Wanaithamini hata kuliko mimi. Kwangu ni heshima na upendeleo mkubwa kuichezea nchi hii," ameongeza.

Ola Aina alikuwa mmoja wa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Nigeria kilichofika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023), ambapo kutokana na kiwango chake bora, alijumuishwa kwenye kikosi bora cha mashindano hayo.