Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba wakimchukua Nwabali itakuwa bomba

NWABALI Pict

Muktasari:

  • Kupata nafasi ya kudumu ya kucheza katika timu ya taifa ya Nigeria huku ukiwaweka nje makipa wanaodaka Ulaya huku wewe ukiwa unacheza klabu za Afrika sio jambo rahisi na linadhihirisha daraja la Nwabali.

KIJIWE kimesikia tetesi Mnyama katika harakati zake za usajili wa dirisha kubwa ameanza kumfuatilia kipa wa mpira, Stanley Nwabali raia wa Nigeria.

Na kikaamua kumpa heshima ya kumuita kipa wa mpira kwa sababu wasifu wake katika soka la Afrika unambeba na ni utambulisho tosha wa daraja lake.

Kupata nafasi ya kudumu ya kucheza katika timu ya taifa ya Nigeria huku ukiwaweka nje makipa wanaodaka Ulaya huku wewe ukiwa unacheza klabu za Afrika sio jambo rahisi na linadhihirisha daraja la Nwabali.

Sasa kwanza tuipongeze Simba kwa ujasiri wa kujaribu uwezekano wa kumnasa kipa huyo ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na Chippa United ya Afrikan Kusini.

Hatuna uhakika kama Simba itamnasa Nwabali lakini ikifanikiwa kwa hilo itakuwa imeua ndege wawili kwa jiwe moja na ni kwamba itapiga bao sana.

Kwanza itakuwa imepata kipa ambaye ataongeza thamani na ubora wa kikosi chao kwa vile ana daraja na uwezo wa juu kuliko makipa wote ambao wapo kwenye kikosi cha Simba hivi sasa.

Kingine itakuwa imempata mchezaji kiongozi ambaye atakuwa msaada mkubwa ndani ya uwanja na katika vyumba vya kubadilishia nguo kutokana na uzoefu wake mkubwa wa kimataifa alionao.

Kama Simba inapata hiyo fursa ya kumsajili Nwabali katika dirisha kubwa lijalo la usajili, haipaswi kuilazia damu na inatakiwa waitumie vizuri waweze kumpata kipa huyo.

Tuwe wakweli tu hakuna klabu ya Tanzania ambayo inaweza kuikataa nafasi ya kumsajili Nwabali huku ikiwa na uhitaji wa mtu wa nafasi hiyo.