Odegaard kubaki Arsenal hadi 2028

LONDON, ENGLAND. MARTIN Odegaard amesaini mkataba mpya Arsenal utakaomweka Emirates hadi 2028. Nahodha huyo anakuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi katika klabu hiyo inayonolewa na Mhispaniola, Mikel Arteta.
Pia kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid anakuwa mchezaji wa sita kwenye orodha ya wachezaji waliosaini mikataba mipya na kuendelea kuitumikia Arsenal kwa muda mrefu.
Arsenal iliwapa mikataba mirefu mastaa kama Bukayo Saka, William Saliba, Gabriel Martinelli, Aaron Ramsdale na Gabriel Magalhaes.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway mwenye umri wa miaka 24 baada ya kusaini mkataba wa kubaki Arsenal alisema: "Jambo la busara kufuata nyayo za Saka, Saliba, Martinelli, Ramsdale na Gabriel Magalhaes ambao tayari walisaini na kubaki hapa."