Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Odegaard kama kawakodi Chelsea

Muktasari:

  • Nahodha huyo wa Arsenal alitengeneza bao la Mikel Merino, ambalo ni pekee lililofungwa kwenye matokeo hayo ya 1-0 iliyopata Arsenal katika kipute hicho kilichofanyika uwanjani Emirates, Jumapili.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO fundi wa mpira, Martin Odegaard anaendeleza rekodi zake tamu kabisa dhidi ya Chelsea tangu alipojiunga na Arsenal.

Nahodha huyo wa Arsenal alitengeneza bao la Mikel Merino, ambalo ni pekee lililofungwa kwenye matokeo hayo ya 1-0 iliyopata Arsenal katika kipute hicho kilichofanyika uwanjani Emirates, Jumapili.

Odegaard alipiga kona iliyounganishwa na Mikel Merino kwa kichwa na kuusukumia mpira huo nyavuni. Hiyo ilikuwa asisti ya tano kwenye Ligi Kuu England dhidi ya The Blues, ikiwa ni pasi nyingi za mabao dhidi ya mpinzani mmoja. Na hilo, ana asisti nyingi dhidi ya Chelsea kuliko mchezaji mwingine yeyote wa Arsenal kwenye historia ya Ligi Kuu England.

Odegaard alikuwa akilingana na mastaa wengine wa Arsenal, Cesc Fabregas na Dennis Bergkamp kwa kuwa na asisti nne dhidi ya timu moja kwenye mechi za Ligi Kuu England, Chelsea - lakini sasa amewavuka wengine na kuweka rekodi zake kuwa pazuri.

Hata hivyo, staa huyo wa Arsenaol bado ana safari ndefu ya kuvunja rekodi ya asisti ya muda wote kwenye ligi inayoshikiliwa na Ryan Giggs. Kwenye mechi 31 za Ligi Kuu England alizocheza dhidi ya Chelsea, gwiji huyo wa Manchester United, Giggs aliasisti mara tisa.

Lakini, kwa Odegaard amekuwa na rekodi tamu kutokana na kukutana na Chelsea mara nane tu kwenye Ligi Kuu England tangu alipojiunga na Arsenal. Na kwenye mechi hizo, Odegaard hajawahi kuonja machungu ya kupoteza dhidi ya Chelsea, huku akifunga mabao mawili jambo linalomfanya awe amehusika kwenye mabao saba ukijumlisha na asisti zake tano.

Na kwa msimu huu hadi sasa, mchango wa Odegaard kwenye kikosi cha Arsenal ni mabao 13 katika mechi 32 alizocheza kwenye michuano yote, huku akiisaidia timu hiyo kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo.

Baada ya kuichapa PSV kwenye hatua ya 16 bora, Arsenal sasa inajiandaa kukipiga na Real Madrid kwenye hatua ya robo fainali.