Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nuno mbioni kupata shavu West Ham United

NUNO Pict

Muktasari:

  • Potter, mwenye umri wa miaka 50, yuko katika hatari ya kufukuzwa baada ya West Ham kupoteza mechi ya tatu mfululizo nyumbani dhidi ya majirani zao wa Jiji la London.

LONDON, ENGAND: KOCHA wa zamani wa Nottingham Forest, Nuno Espirito Santo, ndiye anayependekezwa kuwa mrithi wa Graham Potter ambaye amekalia kuti kavu huko West Ham na muda wowote anaweza kufukuzwa.

Potter, mwenye umri wa miaka 50, yuko katika hatari ya kufukuzwa baada ya West Ham kupoteza mechi ya tatu mfululizo nyumbani dhidi ya majirani zao wa Jiji la London.

Wiki iliyopita, Crystal Palace ilikuwa timu ya tatu mfululizo kutoka London kupata ushindi mbele ya West Ham baada ya Chelsea na Tottenham kuanza.

Kabla ya mchezo wa Palace kuanza, nje ya uwanja wa nyumbani wa West Ham, London Studium kulikuwa na maandamano ya mashabiki ambao walikuwa wakitaka wakurugenzi waondoke na baada ya mechi kumalizika mashabiki hao walihamia kwa Potter wakawa wanaimba kuwa wanataka afukuzwe asubuhi.

Nuno, ambaye alifukuzwa na mmiliki wa Forest, Evangelos Marinakis, mwezi uliopita, anadaiwa kuwa ameshapigiwa hadi simu na mabosi wa West Ham na ameonyesha nia ya kuwa tayari kuchukua mikoba ya Potter.

West Ham ndio ilifanya Mreno huyo afukuzwe, baada ya kuifunga Forest 3-0 katika mechi yake ya mwisho akiwa kocha.

Kocha wa zamani wa West Ham, Slaven Bilic, pia anatajwa kuwa huenda naye akapewa kazi hiyo, pamoja na Sean Dyche na Michael Carrick.

Baada ya mechi dhidi ya Palace, Potter aliulizwa kuhusu hatma yake na kama anaona anapata sapoti kutoka kwa mabosi wa timu hiyo, akasema: "Ndiyo ninapata sapoti, sina sababu ya kudhani sipati sapoti - lakini pia ninaelewa mazingira yaliyopo sasa. Sina malalamiko yoyote kuhusu sapoti ninayopata kutoka kwa viongozi na mashabiki, naamini naweza kubadilisha hali iliyopo sasa, lakini pia ni ngumu. Tuko kwenye hali ngumu, hakuna pa kujificha. Kile pekee unachoweza kufanya ni kukabiliana nacho, tunatakiwa kufanya vizuri kuliko ilivyo sasa."