Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nottingham Forest yasikilizia ofa za Anderson mezani

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Forest inahitaji zaidi ya Pauni 100 milioni ili kumuuza fundi huyu ambaye tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 41 za michuano yote na kufunga mabao mawili.

NOTTINGHAM Forest bado haijapokea ofa rasmi kutoka kwa timu zinazomhitaji kiungo wao, Elliot Anderson, 23, lakini tayari imeanza kujiandaa kisaikolojia kwa uwezekano wa kupokea kubwa kabla ya michuano ya Kombe la Dunia.

Taarifa zinaeleza vigogo vya Ligi Kuu England, Manchester City na Manchester United vyote vinafuatilia kwa karibu maendeleo ya kiungo huyo ambaye ameonyesha kiwango kizuri msimu huu.

Forest inahitaji zaidi ya Pauni 100 milioni ili kumuuza fundi huyu ambaye tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 41 za michuano yote na kufunga mabao mawili.

Kwa sasa inadaiwa yanafanyika majadiliano kati ya wawakilishi wa Elliot na mabosi wa Man City na Man United kabla ya mahasimu wao kuwasilisha ofa rasmi kwenda Forest.

Inaelezwa Elliot anataka kujua kwanza ikiwa Man United itafuzu michuano ya  Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kabla ya kufanya uamuzi. Mkataba wa sasa wa staa huyo unatarajiwa kumalizika 2029.


Morgan Rogers

KIUNGO mshambuliaji wa Aston Villa, Morgan Rogers, 23, anatarajiwa kuwindwa na vigogo wengi Ulaya  dirisha lijalo la majira ya kiangazi. klabu kubwa za Ligi Kuu England zikiwamo Arsenal, Manchester United na Chelsea zimeripotiwa kuonyesha nia ya kumsajili.

Rogers amekuwa katika kiwango bora tangu msimu uliopita hali iliyovutia vigogo wengi barani Ulaya wanaotamani kuipata saini yake. Tovuti ya The Mirror imeripoti Bayern Munich pia inahitaji huduma ya fundi huyu.


Alisson Becker

JUVENTUS  imeanza kupata matumaini ya kumsajili kipa wa Liverpool na timu ya taifa ya Brazil, Alisson Becker, 33, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Ripoti zinaeleza Alisson yuko tayari kutua Ligi ya Italia Serie A, hatua ambayo inaweza kufungua ukurasa mpya katika maisha yake ya soka baada ya mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa na Liverpool.

Mkataba wa sasa wa kipa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu huu amecheza mechi 34 za michuano yote.


James Trafford

ASTON Villa ni miongoni mwa timu zinazopanga kumsajili kipa wa Manchester City,  James Trafford, 23,  dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Trafford, ambaye kwa sasa ni mmoja ya makipa wa timu ya taifa ya England na wanatarajiwa kwenda katika michuano ya Kombe la Dunia awali alitajwa yupo katika rada za Tottenham lakini sasa mambo yanaonekana kuchangamka na Villa inaamini anaweza kwenda kuwa mbadala wa kipa wao wa kimataifa wa Argentina Emiliano Martinez ambaye umri umeshamtupa mkono.


Enzo Fernandez

KIUNGO wa Chelsea, Enzo Fernandez na wakala wake wameomba radhi kwa klabu hiyo kufuatia kauli alizozitoa akiwa kwenye majukumu ya kimataifa na timu ya taifa ya Argentina zilizoashiria uwezekano wake wa  kujiunga na Real Madrid.

Nyota huyo, 25, alitoa kauli hizo zilizoibua mjadala juu ya mustakabali wake hali iliyosababisha apewe adhabu ya kusimamishwa kwa mechi mbili na uongozi wa Chelsea.

Inaelezwa Chelsea itakuwa tayari kumuuza Enzo lakini kwa utaratibu maalum sio kama ambavyo yeye anahitaji.


Christian Kofane

KLABU kubwa za Ligi Kuu England, Liverpool na Manchester City, zimejiunga na Arsenal katika mbio za kuwania saini ya mshambuliaji chipukizi wa Bayer 04 Leverkusen, Christian Kofane, 19.

Taarifa zinaeleza maendeleo yake Leverkusen yamewashawishi maskauti wa klabu hizo ambazo sasa zinafikiria kuwasilisha ofa rasmi.

Arsenal ilikuwa ya kwanza kuonyesha nia, lakini kuingia kwa sasa Liverpool na Manchester City ndio zinaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumpata.


Castello Lukeba

BEKI wa kati wa RB Leipzig, Castello Lukeba anatarajiwa kuondoka ndani ya klabu hiyo dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano.

Staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 23 amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na vigogo kadhaa wa England, ikiwemo Arsenal , Chelsea, Liverpool pamoja na Manchester United.

Taarifa zinaeleza klabu hizo zinaendelea kufanya tathmini ya kina kuhusu uwezekano wa kumsajili Lukeba, ambaye ameonyesha kiwango bora katika Bundesliga tangu msimu uliopita.


Marco Palestra

LIVERPOOL inadaiwa inaongoza katika harakati za kuiwania saini ya beki wa kimataifa wa Italia, Marco Palestra, 21, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika Cagliari Calcio akitokea Atalanta.

Palestra  ambaye anacheza kama beki wa kulia, ameendelea kuonyesha kiwango bora msimu huu hali iliyowavutia maskauti wengi wa timu kubwa za Ulaya ambao wamekuwa Italia kumtazama staa huyo akicheza katika mechi kadhaa.

Kwa sasa Liverpool inafanya mazungumzo na Atalanta kuhusu masuala ya ada ya uhamisho.