Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Noni Madueke ni mshika bunduki

Muktasari:

  • Zaidi ya mashabiki 5,000 walisaini waraka wa kupinga usajili wa staa huyo wakati mara ya kwanza uliporipotiwa, lakini kocha Arteta hakujali na kufanikisha dili hilo kwa ada ya Pauni 48 milioni, ambapo kutakuwa na nyongeza pia ya Pauni 4 milioni.

LONDON, ENGLAND: KUWAKABILI Arsenal msimu ujao mjipange. Ndicho unachoweza kusema baada ya kocha Mikel Arteta kushusha mashine nyingine matata kabisa kwenye kikosi chake baada ya kumnasa winga wa Chelsea, Noni Madueke.

Zaidi ya mashabiki 5,000 walisaini waraka wa kupinga usajili wa staa huyo wakati mara ya kwanza uliporipotiwa, lakini kocha Arteta hakujali na kufanikisha dili hilo kwa ada ya Pauni 48 milioni, ambapo kutakuwa na nyongeza pia ya Pauni 4 milioni.

Madueke, ambaye amefunga mabao 20 katika mechi 92 alizocheza Chelsea, amesaini mkataba kwenye kikosi cha Arsenal ambao utafika ukomo 2030.

Alikuwa kwenye kikosi cha Chelsea kilichokuwa Marekani kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu, lakini aliondoka mapema kabla ya mechi ya fainali dhidi ya PSG ili kukamilisha dili lake la kujiunga na miamba hiyo ya Emirates.

Hata hivyo, Madueke hatakuwapo kwenye ziara ya Arsenal kwenye mechi za pre-season huko Asia, lakini atasubiri hadi mwezi ujao kucheza kwenye Emirates Cup baada ya kumaliza mapumziko yake.

Akielezea kwanini amekubali kujiunga Arsenal, Madueke alisema: “Naamini itakwenda kuwa yenye mafanikio makubwa na nina furaha kuwapo hapa.”

Katika kufahamiana na wachezaji wengi wa Arsenal ambao ni Waingereza wenzake, Madueke alisema: “Nilizungumza na Declan Rice, Myles, Bukayo, na hata Jurrien wote wanasema vitu vizuri kuhusu klabu na utamaduni uliopo. Nimefurahi kuwa familia ya Arsenal kwa sasa. Nasubiri kwa hamu kukutana na vijana mazoezini.”

Saa chache kabla ya uhamisho wake wa kwenda Arsenal kuthibitishwa, Madueke aliposti ujumbe wa kuwaacha Chelsea, alipoandika hivi kwenye Instagram: “Wapendwa Chelsea Football Club, nataka kuwashukuru kwa miaka yote mitatu. Kila mtu aliyehusika katika safari yangu, asante sana. Wachezaji wenzangu, asante, naondoka nikiwa mwenye mapenzi makubwa kwetu jamaa.”

Katika kikosi hicho cha Arsenal, Madueke, ambaye ni staa wa nne kunaswa na Arsenal kwenye dirisha hili, amekabidhiwa jezi Namba 20. Wakati wengine walionaswa na miamba hiyo ya Emirates ni Martin Zubimendi, Christian Norgaard na Kepa Arrizabalaga.