Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nne za Afrika zafuzu 16 bora Kombe la Dunia chini ya miaka 17

U17 Pict

Muktasari:

  • Hatua hii ya 16 bora ni muhimu kwa timu zote, kwani kushinda kutaziwezesha kufuzu hatua ya robo fainali na kuendelea na ndoto ya kushiriki nusu fainali na hatimaye kutwaa taji la dunia kwa vijana chini ya miaka 17.

Nchi nne za Afrika zimefanikiwa kufuzu hatua ya Raundi ya 16 ya Kombe la Dunia la FIFA la Vijana chini ya miaka 17 nchini Qatar.

Hii inafuatia kumalizika kwa mechi za mwisho za hatua ya makundi zilizochezwa jana Jumamosi, Novemba 15, 2025.

Nchi nne zilizofika hatua ya 16 bora katika michuano hiyo ni Uganda, Burkina Faso, Morocco na Mali.

Burkina Faso na Uganda zimefuzu hatua ya 16 baada ya kuifunga Ujerumani na Senegal, mtawalia.

Vilevile, timu kama Uingereza, Italia na Japani zimeungana na wawakilishi wa Afrika baada ya ushindi katika mechi zao za mwisho za hatua ya makundi.

Vilevile, Jamhuri ya Korea iliishinda Venezuela, na Uzbekistan ikaishinda Croatia kwa penalti na kufuzu hatua ya 16 bora.

Hatua ya Raundi ya 16 itaanza Jumanne, Novemba 18, 2025, ambapo Italia itakabiliana na Uzbekistan, Uganda vs Burkina Faso, Mexico dhidi ya Ureno, na Brazil kumalizana na Ufaransa.

Aidha, mechi nyingine ni Switzerland dhidi ya Ireland, Jamhuri ya Korea vs Japan, Austria dhidi ya England, na Morocco ikikabiliana na Mali. Mechi zote zinachezwa kwa muda wa kawaida; iwapo zitafikia sare, matokeo yataamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Hatua hii ya 16 bora ni muhimu kwa timu zote, kwani kushinda kutaziwezesha kufuzu hatua ya robo fainali na kuendelea na ndoto ya kushiriki nusu fainali na hatimaye kutwaa taji la dunia kwa vijana chini ya miaka 17.