Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa kadi nyekundu ya Ronaldo, PFF kuwasilisha malalamiko FIFA

PFF Pict

Muktasari:

  • PFF imepanga kuwasilisha malalamiko kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) kwa lengo la kuomba Ronaldo apunguziwe muda wa adhabu ya kusimamishwa kucheza mechi zinazoratibiwa na shirikisho hilo.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Ureno (PFF), limetoa taarifa ya kutokubaliana na adhabu aliyopewa nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa hilo, Cristiano Ronaldo, kutokana na tabia yake ya ukali wakati Ureno ikifungwa 2-0 dhidi ya Ireland, Novemba 13, 2025.

PFF imepanga kuwasilisha malalamiko kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) kwa lengo la kuomba Ronaldo apunguziwe muda wa adhabu ya kusimamishwa kucheza mechi zinazoratibiwa na shirikisho hilo.

Hata hivyo, jarida la Record linadai kuwa Rais wa PFF, Pedro Proenca, anajiandaa kuwasilisha malalamiko FIFA akitumaini kuepuka adhabu ya zaidi ya mechi moja kwa Ronaldo.

Ripoti hiyo inadai kuwa Ureno itajenga hoja yake kupitia malalamiko hayo kwa mambo matatu.

MAR 02

Hoja ya kwanza ni mazingira ya uhasama jijini Dublin, ambayo PFF inaamini yalichochewa na kocha mkuu wa Ireland, Heimir Hallgrimsson, ambaye hapo awali alimshutumu Ronaldo kwa kumdhibiti mwamuzi katika mechi ya marudiano mjini Lisbon.

Ureno pia inaamini kuwa Ronaldo alichokozwa hadi kupiga kiwiko na alikuwa akivutwa na kushikwa mara kwa mara wakati wa mechi hiyo. 

Pia PFF inaamini kuwa, hakuna rekodi ya awali ya tukio kama hilo kwa Ronaldo, kwani adhabu hiyo ndio ya kwanza kwake katika mechi 226 alizocheza akiwa na timu ya taifa.

Ronaldo atatumikia adhabu ya kadi nyekundu kwa kukosa mechi mbili, ambapo moja kati ya hizo huenda ikawa ile ya kwanza kwa Ureno, endapo itafuzu Kombe la Dunia 2026.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na Juventus, alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumpiga begani kwa kiwiko beki wa Jamhuri ya Ireland, Dara O’Shea.

Ronaldo hatakuwa sehemu ya kikosi cha Ureno kitakachoikabili Armenia, katika mechi ya mwisho ya kufuzu Kombe la Dunia baadae leo Jumapili, Novembva 16, 2025 akianza kutumikia adhabu ya kadi nyekundu.

MAR 01

Sheria za nidhamu za FIFA zinaonyesha kuwa aina ya kadi nyekundu aliyopewa Ronaldo inaweza kumfanya akose angalau mechi mbili au tatu kwa kitendo kilichomsababishia kuadhibiwa.

Ronaldo anatarajiwa kusubiri wiki tatu ili kujua muda kamili wa adhabu yake, kwani FIFA huchukua zaidi ya siku 14, baada ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia kutoa uamuzi wa matukio ya kinidhamu.

Kwa sasa Ureno inaongoza msimamo wa Kundi F, na endapo itaibuka na ushindi dhidi ya Armenia baadae leo Jumapili, itajikatia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia 2026.