Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nigeria yatamba imejiandaa kuinyoosha DR Congo

NIGERIA Pict

Muktasari:

  • Mabao kutoka kwa Victor Osimhen, aliyefunga mawili, huku Akor Adams na Chidera Ejuke yaliipa timu ya kocha Eric Chelle ushindi wa 4-1 dhidi ya Panthers baada ya muda wa ziada katika nusu fainali ya mchujo wa Afrika wa Kombe la Dunia la FIFA 2026.

RABAT, MOROCCO: RAIS wa Shirikisho la Soka Nigeria (NFF), Alhaji Ibrahim Musa Gusau, ametolea maoni ushindi mkubwa wa Super Eagles dhidi ya Gabon usiku wa Alhamisi, huku akitamba timu hiyo imepania kushinda mechi ijayo dhidi ya Dr Congo.

Mabao kutoka kwa Victor Osimhen, aliyefunga mawili, huku Akor Adams na Chidera Ejuke yaliipa timu ya kocha Eric Chelle ushindi wa 4-1 dhidi ya Panthers baada ya muda wa ziada katika nusu fainali ya mchujo wa Afrika wa Kombe la Dunia la FIFA 2026.

Gabon ilipata bao la kufutia machozi kupitia Mario Lemina dakika ya 89, ambalo lilipeleka mchezo hadi muda wa ziada kwenye Uwanja wa Moulay Al Hassan mjini Rabat, Morocco.

MAY 02

“Tumeridhishwa na matokeo,” alisema Gusau, ambaye ameongoza soka la Nigeria tangu mwaka 2022.

“Wachezaji walijitokeza ipasavyo na kuipa Nigeria heshima kwa kucheza vyema.”

Super Eagles sasa watakutana na DR Congo katika fainali ya mchujo wa Afrika Jumapili, huku Leopards wakitwaa ushindi wa 1-0 dakika za mwisho dhidi ya Cameroon katika nusu fainali nyingine iliyopigwa Alhamisi.

MAY 01

“Bila shaka, wana ule ujasiri, uimara na akili ya ushindi kuwashinda yoyote watakayekutana naye kwenye fainali ya Jumapili,” Gusau aliongeza.

Mshindi kati ya Nigeria na Congo atasonga mbele kwa mchujo wa mabara utakaoandaliwa huko Mexico Machi 2026 na iwapo itapenya itaungana na wawakilishi wengine wa Afrika zilizofuzu moja kwa moja ambazo ni Morocco, Tunisia, Algeria, Misri, Ghana, Senegal, Afrika Kusini, Cape Verde na Ivory Coast.