Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nigeria yagonga mwamba, FIFA yatoa orodha ya mwisho Kombe la Dunia 2026

NIGERIA Pict

Muktasari:

  • Tangazo hilo limefuta matumaini madogo ya Nigeria maarufu Super Eagles ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 kupitia ‘mlango wa nyuma’.

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limetoa orodha ya mwisho ya mataifa yatakayochuana katika michuano ya mchujo ya mabara (inter-confederation play-offs), huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) ikitangazwa kuwa mwakilishi pekee kutoka barani Afrika.

Tangazo hilo limefuta matumaini madogo ya Nigeria maarufu Super Eagles ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 kupitia ‘mlango wa nyuma’.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa kuelekea michuano hiyo, FIFA imetaja mataifa sita yatakayoshiriki na kufafanua muundo wa mashindano hayo. Kuingizwa kwa DR Congo kumehitimisha mgogoro wa kisheria ulioanzishwa na Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF), ambalo lilikuwa likipinga matokeo ya mechi ya mchujo wa CAF iliyopigwa Novemba 2025.

Nigeria iliwasilisha malalamiko ikidai kuwa DR Congo iliwachezesha wachezaji wasio na sifa katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 1-1, kabla ya Super Eagles kupoteza kwa mikwaju ya penalti. Hata hivyo, uamuzi wa FIFA wa kutaja orodha ya mwisho unaashiria kuwa rufaa ya Nigeria imegonga mwamba.

Katika taarifa yake, FIFA imesema: "Michuano ya Mchujo ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 itashirikisha timu sita zitakazowania nafasi mbili za mwisho za kufuzu fainali zitakazofanyika nchini Canada, Mexico na Marekani."

FIFA imethibitisha kuwa timu zitakazochuana ni Bolivia, DR Congo, Iraq, Jamaica, New Caledonia, na Suriname.

Mechi hizo za mchujo zinatarajiwa kuanza Machi 26, 2026 ambapo washindi wawili wa kwanza watajipatia tiketi ya kuungana na mataifa mengine kwenye fainali za kihistoria za mwaka 2026.