Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni wikiendi yenye utamu wake

UTAMU Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo inavuta hisia za wengi kuona kama Real Madrid itamaliza uteja wa kuteswa na Barcelona, huku kipute hicho kikibeba hatima ya mbio za ubingwa wa La Liga msimu huu.

BARCELONA, HISPANIA: MAMBO iko kwenye mchakamchaka wa Ligi Kuu za Ulaya, huku kipute cha kibabe zaidi kitakuwa cha El Clasico Jumapili wakati Barcelona itakapokuwa nyumbani na Real Madrid kwenye La Liga.

Mechi hiyo inavuta hisia za wengi kuona kama Real Madrid itamaliza uteja wa kuteswa na Barcelona, huku kipute hicho kikibeba hatima ya mbio za ubingwa wa La Liga msimu huu.

Jumapili, hiyohiyo kwenye Ligi Kuu England kutakuwa na kasheshe la wababe wawili waliokuwa wakifukuzana kwenye mbio za ubingwa, Liverpool itakapokuwa nyumbani kukipiga na Arsenal.

Lakini, wikiendi hii imekuwa ya kibabe sana kwenye ligi kuu tano bora za Ulaya, ambapo mechi nyingine zitakazopigwa Jumapili Ligi Kuu England, Newcastle itaikaribisha Chelsea, wakati Manchester United itaikaribisha West Ham United, Nottingham Forest itaikaribisha Leicester City na Tottenham itamalizana na Crystal Palace.

Kwenye LaLiga, Leganes itacheza na Espanyol, Athletic Bilbao na Alaces ilhali Real Betis na Osasuna.

Bundesliga itashuhudia Bayer Leverkusen itakipiga na Borussia Dortmund, Eintracht Frankfurt na St Pauli huku VfB Stuttgart ikicheza na Augsburg, wakati Serie A Udinese itacheza na Monza, Hellas Verona na Lecce, Torino na Inter huku Napoli ikikipiga na Genoa.

Hata hivyo, kivumbi kitaanza Jumamosi ambapo Ligi Kuu England, Fulham itacheza na Everton, Ipsich Town itakipiga na Brentford, Southampton na Manchester City, Wolves na Brighton na Bournemouth na Aston Villa, wakati La Liga kipute kitakuwa cha Atletico Madrid na Real Sociedad, lakini shughuli nyingine itakuwa kati ya Valencia na Getafe, Celta Vigo na Sevilla, Girona na Villarreal na Mallorca itakipiga na Real Valladolid.

Bundesliga itashuhudia mechi za Holstein Kiel na Freiburg, Union Berlin na Heidenheim, VfL Bochum na Mainz 05, Werder Bremen na RB Leipzig na mabingwa Bayern Munich watakipiga na Borussia Monchengladbach, wakati Serie A kutakuwa na Como itacheza na Cagliari, Lazio na Juventus na Empoli na Parma.

Kwenye Ligue 1 mechi zote zitacheza Jumamosi ambapo AS Monaco itacheza na Lyon, Angers na Strasbourg, Auxerre na Nantes, Brest na Lille, Le Havre na Marseille, Montpellier na PSG, Reims na Saint-Etienne, Rennes na Nice na Toulouse itacheza na Lens.