Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

He! Arsenal hatarini kumaliza namba sita

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Wakati Arsenal ikionekana kujihakikishia kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England kwa msimu wa tatu mfululizo, bado kuna uwezekano wa timu hiyo kumaliza kwenye nafasi ya sita endapo kama matokeo yatakwenda hovyo upande wao kwa wiki mbili zijazo.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL itamaliza msimu mikono mitupu, lakini baada ya kukomea kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia kipigo kutoka kwa Paris Saint Germain, kocha Mikel Arteta sasa atalazimika kuwaweka sawa mastaa wake ili wakamatie pointi mbili wanazozisaka ili kufuzu michuano ya Ulaya msimu ujao.

Wakati Arsenal ikionekana kujihakikishia kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England kwa msimu wa tatu mfululizo, bado kuna uwezekano wa timu hiyo kumaliza kwenye nafasi ya sita endapo kama matokeo yatakwenda hovyo upande wao kwa wiki mbili zijazo.

Kwa sasa Arsenal ina pointi 67 na mechi yao ijayo watakipiga na mabingwa Liverpool, Jumapili kisha watakipiga na Newcastle United inayowania nafasi kwenye Top Five na kuna wasiwasi wa mambo yakawa magumu kwenye kipute cha North London derby kitakachopigwa kati ya sasa hadi Mei 25. Kama Arsenal itanasa pointi mbili kutoka kwenye mechi zijazo dhidi ya Liverpool, Newcastle na Southampton, hapo itakuwa imejihakikishia nafasi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kuwa na wastani mzuri wa tofauti ya mabao ikiwa na mabao 12 juu zaidi ya Newcastle na  Chelsea, 21 dhidi ya Nottingham Forest na 27 dhidi ya Aston Villa.

Lakini, kama itapata pointi moja tu au kukosa kabisa, hilo litafanya kuwa na wakati mgumu zaidi katika kuwania tiketi hiyo ya Ulaya.

Aston Villa itahitaji kushinda mechi zake tatu dhidi ya Bournemouth, Tottenham na Manchester United ili kupata nafasi ya kumaliza juu ya Arsenal huku Forest nayo itahitaji kushinda mechi zote ili kumaliza msimu juu ya kikosi hicho cha kocha Arteta.

Nottingham Forest, yenye pointi 61 na Chelsea iliyopo kwenye nafasi ya tano na pointi 63 ndizo timu zenye nafasi ya kumaliza na pointi 70, hivyo kujiondoa kwenye shaka hiyo, Arsenal inahitaji kukusanya pointi muhimu mapema ili kukamatia tiketi ya Ulaya.